Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice alimaliza ziara yake nchini India na nchini Kazakhstan. Ingawa lengo lake muhimu la kusaini makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyukilia kwa matumizi ya kiraia kati ya Marekani na India katika ziara yake ya India halikuweza kutimizwa, lakini alijitahidi kufanya vizuri kazi ya mshawishi kwa ajili ya makampuni ya tekenolojia ya nyukilia ya Marekani. Bi. Rice alipofanya ziara nchini Kazakstan alisisitiza, lengo la Marekani la kukuza uhusiano na Kazakstan siyo kufanya ushindani na Russia ili kuongeza ushawishi wake kwenye Asia ya kati. Mchambuzi alisema, maneno aliyoyasema Bi Rice siyo ya kutoka moyoni, lengo la ziara yake barani Asia ni kuimarisha maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya Marekani.
Lengo haswa la Bi Rice nchini India ni kusaini makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyukilia kwa matumizi ya kiraia na serikali ya India, ambao uliidhinishwa na bunge la Marekani mwanzoni mwa mwezi huu, na kuufanya mkataba huo kuingia katika kipindi halisi cha utekelezaji. Lakini India iliamua hatimaye kubatili sherehe ya utiaji sahihi kutokana na kwamba rais Bush hakusaini rasmi makubaliano hayo, na kusababisha kushindwa kwa lengo la Bi. Rice. alisema, kuidhinishwa kwa makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyukilia ya matumizi ya kiraia kati ya Marekani na India, kumefanya uhusiano wa Marekani na India uko katika hali iliyotofautiana kabisa na ile ya zamani. Waziri wa mambo ya nje wa India Bw. Pranab Mukherjee alisisitiza pia kuwa uhusiano wa urafiki wa pande hizo mbili umefikia kiwango cha juu kuliko hapo awali, na kweli kabisa umekuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati.
Mchambuzi alisema, ingawa Bi. Rice hakuweza kusaini rasmi makubaliano na India katika ziara yake hiyo, lakini takwimu za Umoja wa viwanda vya India zinaonesha kuwa, katika miaka 15 ijayo, makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyukilia ya matumizi ya kiraia yatajenga vituo 18 hadi 20 vya uzalishaji umeme kwa nishati ya nyukilia kwa ajili ya India, ambavyo uwekezaji utafikia dola za kimarekani bilioni 27.
Baada ya kuondoka India, Bi Rice aliendelea na ziara yake nchini Kazaktan na kuwa na mazungumzo pamoja na viongozi wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano wa nishati na ujenzi mpya wa Afghanistan. Bi. Rice alisema, Marekani haina nia ya kushindana na Russia kuhusu athari kwenye Asia ya kati. Moscow inatilia maanani sana kuhusu ofisa wa Marekani kuitembelea nchi ambayo ilikuwa moja kati ya Jamhuri ya umoja wa Urusi, na iliwahi kuzilaumu nchi za magharibi kujaribu kujenga nguvu za athari katika nchi washirika wake wa jadi. Bi Rice alisema, Marekani kukuza uhusiano na nchi za Asia ya kati hakulengi mtu yeyote, lengo lake siyo kuharibu maslahi ya muda mrefu ya Russia kwenye sehemu ya Asia ya kati. Lakini shirika la habari la Marekani linasema, ni kinyume cha lengo la Bi. Rice, nia yake halisi ni kupunguza athari za Russia kwenye sehemu hiyo.
Tangu kuzuka kwa mapambano kati ya Russia na Georgia, serikali ya Bush ilifanya haraka kuimarisha mawasiliano na nchi za sehemu ya Caucasus na Asia ya kati, na ilitoa ahadi nyingi. Mwezi uliopita, makamu wa rais wa Marekani Bw. Dick Cheney alitembelea Georgia, Ukraine na Azerbaijan. Ziara ya Bi. Rice imezidisha mashaka ya watu kuhusu Marekani kuimarisha nguvu za athari kwenye Asia ya kati.
Mbali na hayo, lengo lingine la Rice katika ziara yake nchini Kazakhstan ni kuimarisha ushirikiano wa nishati na nchi hiyo, ambayo ina maliasili nyingi ya mafuta ya petroli na gesi kwenye sehemu ya bahari ya Caspian. Hivyo lengo la ziara ya Rice nchini Kazakstan ni kwa ajili ya maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya Marekani kwenye sehemu ya Asia ya kati.
|