Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-08 20:12:04    
Umoja wa Ulaya watoa mwito wa kuongeza uratibu katika kutoa msaada wa kuokoa soko la fedha

cri

Hivi karibuni msukosuko wa fedha wa Marekani umeathiri soko la fedha la Ulaya, ambapo mabenki kadha wa kadha makubwa ya Umoja wa Ulaya yamekumbwa na matatizo, na serikali za nchi mbalimbali zililazimishwa kutia mitaji mikubwa kwa mabenki au kuyataifisha ili kuepusha mabenki hayo yasifilisike. Mawaziri wa fedha wa nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya tarehe 7 walifanya mkutano wa kujadili hatua za kukabiliana na msukosuko huo.

Hali halisi ni kwamba, watungaji wa sera wa Umoja wa Ulaya wamekaa macho sana juu ya msukosuko huo wa fedha tangu mwanzo wa kutokea kwake, na watu wanatarajia Umoja wa Ulaya utatoa mpango wa kutoa msaada mkubwa kwa kuokoa soko la fedha kama ule wa Marekani. Lakini nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ni nyingi, ambazo kiwango cha maendeleo ya uchumi, mifumo ya fedha na athari zilizopata zote ni tofauti, na nchi mbalimbali huzingatia zaidi kulinda maslahi yao zenyewe, hivyo si rahisi kupata maoni ya pamoja kwa Umoja wa Ulaya kutoa sera na hatua za kuokoa soko la fedha.

Nchi ya Ufaransa ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya ilipendekeza kutoa mpango kama ule wa Marekani, ambao nchi wanachama zitoe mitaji ya Euro bilioni 350 kwa ajili ya kuokoa soko la fedha, na mpango huo ulitazamiwa kuwasilishwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi nne za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Italia ili ujadiliwe na kuthibitishwa, lakini Ujerumani na Uingereza zilipinga kithabiti mpango huo, hivyo mpango huo ulishindwa kutolewa. Mkuu wa Benki ya Ulaya Bw. Jean-Claude Trichet alisema, hatuna bajeti ya pamoja ya shirikisho, hivyo kuiga njia ya Marekani ya kuokoa soko la fedha hakulingani na miundo ya kisiasa ya Ulaya. Maneno yake hayo yameonesha kuwa, kila nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya inatendea mambo yake yenyewe.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, serikali ya Ireland ilitangaza kwa upande wake mmoja kuwa itatoa dhamana kwa miaka miwili kwa ajili ya akiba zote za mabenki ya nchi hiyo ili kutuliza soko la fedha la nchi hiyo, hatua hiyo ililaumiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kama vile Uingereza na Ujerumani, ambazo zinahofia kwamba hatua hiyo itasababisha kupoteza kwa akiba ya benki za nchi zao. Juu ya hiyo, mkutano wa wakuu wa Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Italia uliofanyika tarehe 4 ulisisitiza zaidi kuwa, nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Ulaya zinapochukua hatua za kuokoa soko la fedha zinapaswa kuzingatia athari isiyofaa kwa nchi jirani zake. Lakini siku ya pili baada ya mkutano huo, Ujerumani ilitangaza mpango wake wa kutoa dhamana kwa akiba zote za benki nchini humo kama ilivyofanya Ireland. Baada ya hapo, nchi nyingine mbalimbali zilifanya vivyo hivyo na kutoa hatua za kulinda maslahi ya wateja wa benki, ambapo soko la akiba la benki la Umoja wa Ulaya limezidi kuwa na hali isiyo ya utaratibu.

Mkutano wa mawaziri wa fedha ulofanyika tarehe 7 umetoa "kanuni za uelekezaji" kuhusu hatua za nchi mbalimbali za kuokoa soko la fedha, lakini bado ulisisitiza kuwa hatua za serikali za kila nchi ziamuliwe na nchi hizo, lakini nchi mbalimbali zinapaswa kuratibu vitendo vyao kwa karibu, na kuzingatia kwa makini athari itakayosababishwa na hatua zao kwa nchi nyingine.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, kadiri msukosuko wa fedha unavyozidi kuwa mkali, nchi wananchama wa Umoja wa Ulaya zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na msukosko, kama Umoja wa Ulaya hauwezi kuchukua hatua halisi ya kusawazisha vitendo, mustakabali wa uchumi wa Umoja wa Ulaya hautafurahisha. Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika katikati ya mwezi huu ambao ni wa mara ya mwisho wa mwaka huu unatakiwa kutambua hali halisi ya mambo ili kutoa hatua halisi ya kuokoa soko la fedha kwa ajili ya nchi wanachama wake.