Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-08 20:25:16    
Mapishi ya slesi ya nyama ya nguruwe na uyoga

cri

Mahitaji:

Nyama ya nguruwe gramu 200, uyoga gramu 100, nusu ya pilipili mboga, wanga nusu ya kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, ute wa yai moja, chumvi vijiko viwili, na tangawizi

Njia:

1. kata nyama ya nguruwe, uyoga na pilipili mboga ziwe slesi, koroga slesi ya nyama ya nguruwe pamoja na wanga, mchuzi wa sosi, ute wa yai na maji kidogo.

2. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria halafu tia slesi ya nyama, korogakoroga, tia slesi ya uyoga na vitunguu saumu, korogakoroga tia slesi ya pilipili mboga, tia chumvi korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.