Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-10 17:35:12    
Napenda Beijing!

cri
Balozi wa China nchini Marekani Bw. Zhou Wenzhong hivi karibuni alifanya tafrija kubwa ya kupongeza mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, na kushukuru uungaji mkono mkubwa na ushirikiano wa watu wa sekta mbalimbali wa Marekani kwa China katika kuiandaa Michezo ya Olimpiki. Watu walioalikwa kwenye tafrija hiyo walieleza kuwa, Michezo ya Olimpiki ya Beijing si kama tu ni michezo mikubwa, bali ni shughuli kubwa zaidi za mawasiliano ya utamaduni kati ya China na dunia, na kuwafanya watu wengi zaidi kuifahamu China.

Naibu waziri wa fedha wa Marekani Bw. Robert Kimmit, naibu waziri wa mambo ya nje Bi. Paula Dobriansky, mwenyekiti wa Kamati ya uhusiano kati ya Marekani na China Bi. Carla Hills, mjumbe wa Kamati ya Olimpiki ya Marekani Bw. John Hendricks, na balozi wa zamani wa Marekani nchini China Bw. James Sasser pamoja na wamarekani wa sekta mbalimbali, na wachina wanaoishi nchini Marekani na wanafunzi wa China wanaosoma nchini humo zaidi ya 500 walialikwa kwenye tafrija hiyo.

Kwenye tafrija hiyo, balozi Zhou Wenzhong alikumbusha siku 16 za Michezo ya Olimpiki ya Beijing ambazo ziliwapa watu picha nzuri. Alieleza kuwa michezo hiyo imeonesha moyo wa Olimpiki ulio wa umoja, urafiki, amani na maendeleo. Alisema:

"Mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing si kama tu yanategemea uungaji mkono wa wananchi wa China, na mafanikio yaliyopatikana katika miaka 30 iliyopita tangu China itekeleze mageuzi na ufunguaji mlango, bali pia ni matokeo ya juhudi za pamoja za nchi mbalimbali duniani. Fahari tuliyo nayo vilevile ni kwa familia kubwa ya Olimpiki ya Kimataifa, na inapatikana kutokana na juhudi za wachezaji wa nchi mbalimbali na watu laki kadhaa wa kujitolea wa Michezo ya Olimpiki na watu waliohudumia michezo hiyo kwa njia mbalimbali. Nataka kutumia fursa hii kutoa salamu za pongezi kwa ujumbe wa Marekani wa Michezo ya Olimpiki kutokana na mafanikio yake yaliyopatikana, na kutoa shukurani kwa uungaji mkono mkubwa wa serikali na wananchi wa Marekani. Rais George Bush wa Marekani na ujumbe wa ngazi ya juu kushiriki kwenye ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, ni uungaji mkono kwa China ambayo ni nchi mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, na kwa moyo wa Olimpiki."

Watu wa hali mbalimbali wa Marekani walipongeza mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Mwenyekiti wa Kamati ya uhusiano kati ya Marekani na China Bi. Carla Hills alisema, Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeweka alama mpya kwenye historia ya michezo hiyo, akisema:

"Juhudi za miaka saba zimeifanya Beijing kuiletea dunia nzima michezo mizuri zaidi ya Olimpiki katika historia ya michezo hiyo. Wananchi wa China wana sababu za kutosha za kuona fahari kutokana na michezo hiyo. Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeonesha usanii murua na majengo mazuri, pamoja na urafiki mkubwa wa wananchi wa China kwa watu wa dunia nzima, na kuisukuma China kwenye kituo cha kiini cha jukwaa la dunia. Nawaonea wananchi wa China fahari kubwa."

Mjumbe wa Kamati ya Olimpiki ya Marekani Bw. John Hendricks alisema, hamu ya watu wa nchi mbalimbali duniani kwa michezo inaongezeka kutokana na Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Alitoa mfano, thuluthi mbili ya watu duniani walitazama Michezo ya Olimpiki ya Beijing, na idadi hiyo imefikia bilioni 4.7, na nchini Marekani michezo hiyo iliwavutia watazamaji milioni 200 wa televisheni, na kuwa mashindano yaliyowavutia watazamaji wengi zaidi katika historia ya televisheni nchini humo. Bw. Hendricks alisema:

"Mafanikio makubwa zaidi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni urafiki wa watu wa China kwa wachezaji na watalii kutoka nchi mbalimbali duniani. Urafiki huu ulijaa tangu mwanzo hadi mwisho wa michezo hiyo, pia umesogeza karibu uhusiano kati ya wachezaji na watazamaji. Wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya Marekani na ujumbe wa Michezo wa Olimpiki ya Marekani walipoondoka mjini Beijing, walikuwa na urafiki mkubwa na watu wa China, na urafiki huo utadumishwa katika siku za baadaye."

"Nimeishi nchini China kwa siku 17, na niliishi mjini Beijing kwa siku 6. Nataka kusema napenda Beijing."

Kocha wa mpira wa tennis Bi. Kathy Kemper alipigwa makofi kwa furaha kutokana na maneno aliyoyasema kwa lugha ya kichina "Napenda Beijing." Yeye na jamaa zake walitembelea mitaa na vichochoro mjini Beijing. Alisema ingawa ameshiriki kwenye mashindano mengi ya michezo katika sehemu mbalimbali duniani, lakini Michezo ya Olimpiki ya Beijing inamfanya ajisikie mengi ambayo hakuyapata zamani. Alisema:

"Vivutio vya China vinajulikana duniani, lakini wamarekani wengi hata watu wengi wa nchi za magharibi bado hawafahamu vizuri watu wa China. Wachina niliwakuta, ama wakazi wa Beijing au watu waliojitolea wa Michezo ya Olimpiki, wanapenda kufanya mawasiliano na watu wa nchi za nje, na wana furaha,ukarimu na majivuno, na hayo sijahisia zamani kwenye sehemu nyingine. Wachina wana wazo la ufunguaji, na wanapenda kujifunza kutoka kwa wengine, pia wanaonesha uchangamfu mkubwa kwa watalii. Walitia moyo kwa wachezaji wa nchi yao wenyewe, vilevile kwa nchi nyingine duniani. Nataka kusema wamepata medali muhimu zaidi ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki. Napenda Beijing."