Ili kukabiliana na msukosuko wa fedha kwa pamoja, na kuhimiza ongezeko la uchumi, benki kuu ya Ulaya pamoja na benki kuu za nchi nyingine za Ulaya na Marekani tarehe 8 zilipunguza faida ya akiba zilizowekwa benkini kwa basic point 50, hatua hiyo imeshangiliwa mara moja na sekta mbalimbali. Lakini sasa ni vigumu kubashiri kiwango cha imani kuhusu masoko kinachoweza kurejeshwa pamoja na muda wake.
Katika siku hiyo, benki kuu za Ulaya zilipunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini hadi 3.75% kutoka 4.25%, wakati kamati ya hazina ya shirikisho la majimbo ya Marekani, benki kuu ya Canada pamoja na benki kuu za nchi nyingine za Ulaya, Uingereza, Usiwis na Swiden zililipunguza pia faida ya fedha zilizowekwa benkini.
Taarifa iliyotolewa na benki kuu ya Ulaya inasema, msukosuko wa fedha inayozidi hivi sasa imeongeza hatari ya kudhoofika zaidi kwa uchumi wa nchi zinazotumia Uro, lakini vilevile imepunguza hatari ya kuzidi kwa mfumuko wa bei. Hivyo benki kuu ya Ulaya pamoja na benki kuu nyingine zimeamua kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini.
Uamuzi wa kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini wa benki kuu ya Ulaya umekaribishwa sana na nchi zinazotumia Uro, hususan nchi za Ufaransa na Ujerumani, ambazo zimekuwa zikidai benki kuu ya Ulaya kulegeza sera za sarafu. Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alisema, hatua hiyo inachangia ustawi wa uchumi wa nchi zinazotumia Uro. Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Bw. Michael Glos alisema, kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini ni hatua moja sahihi iliyochukuliwa.
Katika muda mrefu uliopita, benki kuu ya Ulaya ilichukulia kutuliza bei za vitu katika nchi zinazotumia Uro kama ni sera muhimu za sarafu. Mwaka huu, pamoja na kupanda kwa bei za nishati duniani pamoja na bei za chakula, nchi zinazotumia Uro zilikabiliwa na hali mbaya ya mfumuko wa bei, ambayo ilifikia 4.25% kutoka 4%. Lakini kiwango cha juu cha faida ya fedha zilizowekwa benkini licha ya kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, vilevile kimedhoofisha uwekezaji na ununuzi wa bidhaa, na kuzidisha matatizo ya uchumi wa nchi zinazotumia Uro.
Kwa kukabiliwa na tishio la kuzorota kwa uchumi na mfumuko wa bei za vitu pamoja na shinikizo kubwa nchi zinazotumia Uro kutaka kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini, katika kipindi fulani kilichopita, benki kuu ya Ulaya iliingia hali isiyokuwa na mbele wala nyuma. Lakini, pamoja na kupungua kwa bei ya mafuta ya petroli duniani, upandaji wa bei za vitu katika nchi zinazotumia Uro ulipungua katika miezi miwili iliyopita, ambao ulifikia hadi 3.6% katika mwezi Septemba, hata hivyo bado umezidi kiwango cha usalama cha 2% kilichowekwa na beki kuu ya Ulaya, lakini hali ya kupungua kwa bei za vitu imeanzisha mazingira ya kupunguza vizuizi kwa utoaji mikopo ya benki. Ni dhahiri kwamba msukosuko wa fedha inayoathiri barani Ulaya imeilazimisha benki kuu ya Ulaya kufanya uamuzi hatimaye kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini.
Lakini, mwitikio wa masoko kuhusu hatua iliyochukuliwa na benki kuu mbalimbali unawashangaza watu. Tarehe 8 mwezi huu, thamani ya hisa kwenye masoko makubwa ya hisa ya Ulaya iliendelea kupungua. Hali mbaya zaidi ni kuwa hadi hivi sasa Umoja wa nchi za Ulaya bado haujaweza kutoa mkakati wa kukabiliana na msukosuko wa fedha, hali ambayo huenda itapunguza ufanisi wa hatua iliyochukuliwa na benki kuu ya Ulaya ya kupunguza faida ya fedha zilizowekwa benkini. Hivyo, pande mbalimbali zinataka mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika tarehe 15 mwezi huu upige hatua halisi ili kuhakikisha nchi za Umoja wa Ulaya zisawazishe hatua zeke na kukabiliana na matatizo kwa pamoja.
|