Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-13 15:53:45    
Serikali ya Xinjiang yatoa mafunzo kwa vijana wa makabila madogo madogo 

cri

Kati ya watu wanaoishi vijijini katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang, watu wa makabila madogo madogo ni wengi sana, na hasa katika sehemu za Hetian na Kashen zilizoko kusini mwa mkoa huo, wakulima na wafugaji wa makabila madogo madogo wanachukua asilimia zaidi ya 95 ya idadi ya watu wote. Ili kuboresha maisha ya watu hao wa makabila madogo madogo, kuanzia mwaka 2006 serikali ya mkoa wa Xinjiang iliwahimiza baadhi ya nguvukazi vijijini kufanya vibarua katika miji mikubwa nchini China, na kuwatolea mafunzo mbalimbali ya ajira.

Tarehe 27 ya mwezi Machi mwaka huu, watu wengi walikuwa wanakusanyika katika mtaa mmoja wa wilaya ya Shufu iliyoko kusini mwa mkoa wa Xinjiang, kwani wanaume 50 na wake wao walikuwa watakwenda kufanya kazi za vibarua mijini baada ya kumaliza mafunzo husika, na jamaa na marafiki zao walikusanyika kuwasindikiza kutoka sehemu za mbali. Mzee Yusup Sulayman wa kabila la Wauyghur alikuwa anawasindikiza watoto wake, alisema,

"Mwezi Novemba mwaka jana, mtoto wa jamaa yangu mmoja alikwenda kufanya kazi za vibarua mjini Tianjin. Kwa kupitia mazungumzo kwenyemtandao wa Internet, niliona mazingira mazur ya maisha yake. Hivyo safari hii nilikubali binti yangu na mume wake waende mjini kufanya kazi za vibarua. Ni vizuri kwao kwenda nje pamoja, kwa kuwa wataweza kusaidiana na kuishi kwa masikilizano."

Kutokana na athari ya mila na desturi ya jadi, zamani watu wa makabila madogo madogo wanaoishi kusini mwa mkoa wa Xinjiang hawakupenda mabadiliko na kukataa kuondoka nyumbani. Ili kuwasaidia watu hao, serikali ya mkoa wa Xinjiang iliandaa mafunzo kwa vijana wasio na kazi, na kupiga fulamu kuhusu maisha ya vijana wanaofanya kazi za vibarua katika miji mbalimbali nchini China, na kuzionesha kwa wazazi wao. Baada ya kujionea maisha mazuri ya vijana hao, maoni ya watu wa sehemu hiyo yalibadilika. Mzee wa kabila la Wauyghur Bw. Iminhasan Mamut alisema,

"Zamani tukipata chakula tuliridhika, na baada ya kuona maisha ya watu wa mijini yalivyo, tumejua kuwa tunaweza kufanya kazi nyingi nzuri mbali na kilimo. Maoni yetu ya zamani ya kupoteza wakati bila kufanya lolote kweli si mazuri."

Bw. Burjahan Ismayil ni mkulima wa sehemu ya Hetian kusini mwa mkoa wa Xinjiang, na ni mmoja kati ya watu walioanza kufanya kazi za vibarua mijini mapema. Alisema kufanya kazi za vibarua mijini kumebadilisha sana maisha yake, alisema,

"Mashamba ni msingi wa maisha yetu, lakini mbali na kulima mashamba, tunaweza kuboresha maisha yetu kwa njia nyingine."

Haifai kufanya wakati ipite bure, sasa vijana wengi wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang wanaona kuwa wanapaswa kujifunza elimu nyingi na kupata uwezo wa ajira.

Sasa katika sehemu mbalimbali kusini mwa mkoa wa Xinjiang, ukitembelea darasa lolote la mafunzo ya ajira, utawaona wanafunzi wakijifunza elimu na ufundi kwa bidii. Katika madarasa hayo, wanaweza kujifunza ufundi mbalimbali wanaotaka zikiwemo nakshi, ufumaji wa blangeti, uchongaji wa sanamu za ubao, utengenezaji wa vitu vya sanaa na uchoraji. Katika kijiji kimoja cha sehemu ya Kashen mkoani Xinjiang, wanakijiji 520 wanashughulikia kutengeneza alaza muziki za kikabila. Wanaweza kutengeneza ala za muziki za aina zaidi ya 50, na ala hizo zinauzwa hata katika nchi za nje zikiwemo Japan, Marekani na nchi za ulaya.

Kwa wakulima vijana wa mkoa wa Xinjiang, kuondoka nyumbani na kuacha kazi za kilimo si kama tu kuongeza mapato, bali pia kunabadilisha mtindo wa maisha yao, na vijana hao waliofanya kazi mijini wameona dunia ya nje na kuzoea maisha mijini. Ili kuwasaidia na kuwahudumia watu hao wanaofanya kazi za vibarua mijini, serikali za sehemu mbalimbali za mkoa wa Xinjiang zilisaini makubaliano ya ajira na miji mikubwa nchini China, na kuanzisha uhusiano wa muda mrefu wa ajira.

Hivi sasa, katika tarafa na wilaya mbalimbali za sehemu za Kashen, Hetian na Kesulezi, vijana wanaofanya kazi za vibarua mijini wanaongezeka siku hadi siku. Vijana hao walishinda matatizo mbalimbali, na kufanya kazi vizuri. Mzee kutoka kabila la Wakirghiz Bw. Tohtar Yusup alisema,

"Naishi katika uwanda wa juu wa Pamir ulioko magharibi zaidi mwa China. Katika sehemu hiyo, asilimia zaidi ya 90 ya ardhi ni ya milima, hakuna mashamba ya kulimwa, wala nyasi za kwa ajili ya malisho kwa mifugo, hatuwezi kubadilisha maisha yetu ila tu kuwahimiza watoto wetu kufanya kazi za vibarua mijini."

Hivi sasa serikali ya mkoa wa Xinjiang inawahimiza sana vijana wa makabila madogo madogo mkoani humo kuanzisha shughuli katika miji iliyoendelea ya mikoa mingine, na pia imewaongezea nafasi za ajira mkoani humo. Vitu vyenye umaalumu wa mkoa wa Xingjiang zikiwemo sanaa za ufumaji wa blangketi, utengenezaji wa visu, ufumaji wa nyuzi za hariri, na vyakula vya makabila madogo madogo vilipata matuzo katika maonesho ya chapa nzuri ya nguvukazi ya China, na kuanzisha mazingira mazuri kwa vijana wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang kupata ajira.

Imefahamika kuwa katika miaka kati ya mitatu na mitano ijayo, serikali ya mkoa wa Xinjiang itatilia mkazo wa kuwahimiza watu wa mkoa huo wapate ajira nzuri zaidi, na kuwaandalia semina za kuongeza mapato na kutafuta ajira. Inakadiriwa kuwa baadaye katika miji mbalimbali nchini China, watu wanaofanya kazi za vibarua kutoka mkoa wa Xinjiang wataongezeka zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2008-10-13