|
Baada ya mkutano wa wakuu wa nchi zinazotumia fedha ya Euro kupitisha mpango wa vitendo wa kusaidia benki kukusanya mitaji, nchi zinazotumia Euro zilitoa sera kamili tarehe 13 ili kuokoa masoko, Euro trilioni 1 zitaongeza imani ya watu juu ya masoko ya fedha ya Ulaya na ya dunia. Mpango huo kabambe wa kuokoa masoko ya fedha hatimaye utaweza kukomesha duru hilo la msukosuko wa fedha.
Viongozi wa nchi 15 zinazotumia Euro tarehe 12 huko Paris walipitisha mpango wa vitendo wa kuokoa masoko ya fedha, serikali za nchi hizo zitatoa dhamana kwa hati zenye thamani zilizotolewa na benki au kununua moja kwa moja hisa za benki, ili kusaidia benki kujipatia mitaji mingi zaidi na kupunguza matatizo ya ukusanyaji fedha yaliyosababishwa na kupunguzwa kwa utoaji wa mikopo ya benki.
Kutokana na mpango huo wa vitendo, nchi muhimu zinazotumia Euro tarehe 13 zilitangaza hatua zitakazochukuwa. Lakini masoko ya hisa ya Ulaya yalikuwa katika hali mbaya kabisa wiki iliyopita, hivyo, mpango huo kabambe unachukuliwa na watu kuwa umechelewa. Ukweli ni kwamba tangu duru hilo la msukosuko wa mambo ya fedha kuenea hadi Ulaya, nchi za Umoja wa Ulaya zilichukua hatua za kuuzuia usiathiri vibaya masoko yake, lakini hazikupata ufanisi mzuri katika kuimarisha imani ya watu juu ya masoko kutokana na kuwa toka mwanzoni kila nchi ilijitegemea yenyewe. Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya, Bw. Jose Manuel Barroso alipotoa hotuba alisisitiza mara nyingi kwamba nchi wanachama wa umoja huo zinatakiwa kuimarisha mashauriano ili kuweka mpango wa pamoja wa kukabiliana na msukosuko wa fedha.
Tarehe 13, nchi zinazotumia Euro zilipotangaza mpango wa kuokoa masoko ya fehda, masoko matatu makubwa ya hisa ya Ulaya yaliingia katika hali nzuri, kiwango cha ongezeko katika siku hiyo kilifikia 10%, wakati masoko ya hisa ya Marekani pia yalikuwa na ongezeko kubwa. Lakini wachambuzi walisema, ongezeko la muda la masoko ya hisa ya dunia lilitokana na sababu nyingi ikiwemo ya serikali za nchi mbalimbali kuukabili msukosuko wa utoaji mikopo kwa ushirikiano. Ingawa mpango wa kuokoa masoko ya fedha ya nchi za Ulaya ulifanya kazi muhimu katika kuimarisha imani ya watu juu ya masoko, lakini majibu ya watu juu ya mpango wa Marekani wa kutoa dola za kimarekani bilioni 700 kuokoa masoko ni kwamba bado haijaweza kuona wazi kuwa hatua hiyo itaweza kweli kudhibiti ipasavyo msukosuko wa fedha na msukosuko wa masoko ya hisa unaozidi kuwa mbaya.
Takwimu inaonesha, katika wiki iliyopita thamani ya hisa kwenye masoko yote ya dunia iliingia hewani kwa dola trilioni 6, na hasara ya thamani ya hisa kwenye masoko yote ya dunia imefikia kiasi cha dola za kimarekani trilioni 27 ikihesabiwa kutoka mwanzoni mwa mwaka huu. Hivyo wachambuzi wanasema, sasa haijulikani kama mpango wa kuokoa masoko wa nchi za Umoja wa Ulaya utaweza kujenga imani ya watu katika muda mrefu ujao, kwani hasara ya wawekezaji ni halisi, kuokoa masoko kwa serikali ni msimamo tu, ambao unaonesha nia na imani ya nchi za umoja huo katika kukabiliana na msukosuko wa fedha. Wanauchumi wamesema, lengo la Umoja wa Ulaya la kuokoa masoko ni kutarajia matatizo mbalimbali yanayoyakumba mashirika ya fedha, yasienee hadi katika uchumi wa taifa.
Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa sasa ya Umoja wa Ulaya, tarehe 13 alipotangaza mpango wa Ufaransa wa kuokoa masoko ya fedha alisema, hatari kubwa zaidi bado haijafika. Mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Ulaya wa majira ya Autoum utakaoanza tarehe 15 utajadili zaidi kuhusu msukosuko wa mambo ya fedha, ambapo masoko pia yanatarajia Umoja wa Ulaya utachukua hatua zinazofuata za kuokoa masoko.
|