Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-15 16:30:33    
Syria yatangaza kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon

cri

Tarehe 14 Rais wa Syria Bw. Bashar al-Assad alitangaza amri ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon. Hii inadhihirisha kuwa Syria imeitambua Lebanon kuwa ni nchi huru, lakini kuufanya uhusiano wa pande mbili uwe wa kawaida kunahitaji muda.

Amri ya rais imesema amri hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia siku ya tangazo. Imefahamika kwamba waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Bw. Fawzi Salloukh tarehe 15 atafanya ziara nchini Syria na kujadiliana na waziri wa mambo ya nje wa Syria kuhusu mambo halisi ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi.

Kuhusu taarifa ya Syria kutaka kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon, pande mbalimbali nchini Lebanon ziliitikia kwa juhudi. Rais wa Lebanon Bw. Michel Sulaiman na waziri mkuu Bw. Fuad Siniora wote wanatumai kwamba sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utafungua ukurasa mpya. Bw. Walid Jumblatt ambaye ni mmoja wa viongozi wa wabunge walio wengi alisema kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi ni mwanzo wa uhusiano mzuri kati ya Lebanon na Syria. Bw. Mohammad Fneish ambaye ni mpinzani ndani ya bunge la Lebanon na mwanachama wa chama cha upinzani cha Hezbollah alisema, hatua ya Syria inaonesha kwamba Syria kweli inataka kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon.

Wachambuzi wanaona kuwa tokea miaka ya 40 ya karne iliyopita nchi hizo mbili zilipotangaza uhuru, Syria siku zote ilikuwa inaona Lebanon ni sehemu yake na haitambui kama ni nchi huru, kwa hiyo ilikataa kuweka uhusiano wa kibalozi nayo. Mwaka 1976 Syria ilituma jeshi kuikalia Lebanon na kuidhibiti kwa miaka takriban 30 mpaka Aprili mwaka 2005 jeshi hilo lilipoondoka kabisa.

Kufuatia utatuzi wa msukosuko wa kisiasa nchini Lebanon, uhusiano mbaya uliosababishwa na kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Bw. Rafiq Hariri ulianza kulegea. Mwezi Agosti mwaka huu Rais wa Syria Bw. Bashar al-Assad alikutana na Rais wa Lebanon Bw. Michel Sulaiman aliyekuwa ziarani nchini Syria, katika mji wa Damascus walitangaza kwamba nchi hizo mbili zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Taarifa rasmi ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon imedhihirisha kuwa Syria inaitambua Lebanon kuwa ni nchi kamili, hatua hiyo itasaidia nchi hizo mbili kuweka uhusiano wa "kuheshimiana na kunufaishana" na pia itasaidia kuleta hali ya usalama na utulivu katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Aidha, hatua hiyo pia itasaidia kulegeza uhusiano mbaya uliosababishwa na kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Bw. Rafiq Hariri kati ya Syria na nchi za Magharibi na kuvunja hali ya kutengwa. Ukweli ni kwamba kufuatia utatuzi wa msukosuko wa kisiasa nchini Lebanon na uhusiano mbaya ulivyobadilika kuwa mzuri kati ya Syria na Lebanon, uhusiano kati ya Syria na Ufaransa umekuwa mzuri kwa kiasi kikubwa.

Wachambuzi wanaona kuwa ingawa Syria imetangaza ni ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Lebanon, kuufanya uhusiano huo uwe mzuri na kudumu kunahitaji muda mrefu. Sababu ni kwamba, kwanza Syria iliwahi kuidhibiti Lebanon kwa miaka 30, matatizo kati ya nchi hizo mbili yako mengi na kuyatatua matatizo hayo kunahitaji muda; Pili, uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaathirishwa na makundi tofauti ya kisiasa kutoka nchini Lebanon na nchi za nje. Wapinzani walio wengi ndani ya bunge la Lebanon na Marekani na nyingine za Magahribi zinazowaunga wapinzani hao siku zote wanataka kuondoa athari ya Syria nchini Lebanon. Baada ya Hezbollah yenye uhusiano mzuri na Syria kupata haki ya hapana dhidi ya serikali katika bunge, mapambano kati yake na makundi ya upinzani yataendelea, na namna ya kushughulikia uhusiano na Syria itakuwa kiini cha mapambano yote nchini Lebanon.

Idhaa ya kiswahili 2008-10-15