Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-15 16:59:08    
Mapishi ya nyama na pilipili boga na pilipili hoho

cri

Mahitaji: Nyama ya ng'ombe gramu 300, pilipili boga gramu 150, pilipili hoho gramu 150, vitunguu saumu gramu 10, mchuzi wa sosi vijiko viwili, wanga kijiko kimoja, sosi ya chaza vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja.

Njia:

1.kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, changanya pamoja na wanga, mchuzi wa sosi na mafuta. Kata pilipili boga na pilipili hoho ziwe vipande?

2.washa moto, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga, halafu tia vipande vya vitunguu saumu, pilipili hoho na pilipili boga, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi na sosi ya chaza, chembechembe za kukoleza ladha na chumvi, korogakoroga,ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.