Tarehe 16 mwezi Okatoba mwaka huu ni "siku ya nafaka duniani" ya mwaka wa 28. Shirika la nafaka na kilimo duniani, FAO, limebuni kauli-mbiu ya siku ya nafaka ya dunia ya mwaka huu kuwa ni "usalama wa nafaka duniani: changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na nishati ya mimea", likitarajia watu wazingatie zaidi changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa na nishati ya mimea.
Mabadiliko ya hali ya hewa yanamwathiri kila mtu hasa kwenye masuala ya nguo, chakula, makazi na mawasiliano, lakini wale wanaoathiriwa vibaya zaidi ni wakulima, wavuvi na watu wanaopata riziki yao kutoka misituni. Mafuriko ya maji na ukame vilivyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa vinaathiri uzalishaji wa nafaka, na kuleta changamoto dhidi ya usalama wa nafaka duniani. Shirika la FAO linaona, kilimo kinafanya kazi mbili katika mchakato wa mabadiliko ya hali ya hewa, kwa upande mmoja shughuli za kilimo zinaweza kutoa hewa inayoongeza joto duniani, lakini kwa upande mwingine zinatoa mchango katika kupunguza utoaji wa hewa inayoongeza joto la dunia. Takwimu iliyotolewa na shirika la FAO inaonesha kuwa utoaji wa hewa inayoongeza joto la dunia katika shughuli za kilimo na ukataji miti ovyo unachukua zaidi ya 30% ya ile ya jumla ya utoaji wa hewa ya aina hiyo duniani, lakini endapo watu watabadilisha mtindo wa uzalishaji mali kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira ya asili, kama vile, kupunguza ukataji miti ovyo, kuboresha hifadhi ya misitu na kudhibiti mtindo wa kulisha mifugo malishoni, basi watu wengi zaidi watapata shibe.
Mbali ya hayo, katika miaka ya karibuni maendeleo ya kasi ya kazi za viwanda ya nishati ya mimea ya duniani, nishati ya mimea imekuwa mbinu moja ya kupunguza utoaji wa hewa inayoongeza joto duniani na kiwango cha kutegemea nishati ya asili. Hali hiyo imeleta changamoto nyingine kwa usalama wa nafaka duniani. Mwezi Juni mwaka huu, wajumbe wa nchi 181 na jumuiya za kimataifa kumi kadhaa pamoja na wakuu wa nchi 43 walishiriki mkutano wa ngazi ya juu kuhusu usalama wa nafaka wa dunia, kauli-mbiu ya mkutano huo ni sawa kabisa na ile ya "siku ya nafaka duniani". Katika mkutano huo, uhusiano kati ya nishati ya mimea na usalama wa nafaka ulikuwa suala lenye mgongano mkali wa misimamo.
Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na shirika la FAO ya "hali ya nafaka na kilimo mwaka 2008" inasema, ili kutimiza usalama wa nafaka duniani, kulinda wakulima maskini, kuhimiza maendeleo ya pande mbalimbali ya sehemu za vijijini na kuhakikisha maendeleo endelevu ya mazingira, tunapaswa kutathimini upya sera kuhusu nishati ya mimea. Taarifa hiyo inasema, kati ya mwaka 2000 na mwaka 2007, uzalishaji wa nishati ya mimea unaotumia mazao ya kilimo uliongezeka kwa mara 3, ikichukua 2% ya nishati zinazotumiwa na vyombo vya usafirishaji duniani, isitoshe uzalishaji huo bado utaendelea kuongezeka. Hata hivyo, mchango unaotolewa nao bado ni mdogo sana kuhusu nishati ya dunia, lakini mahitaji ya uzalishaji nishati ya mimea juu ya mazao ya kilimo yataendelea kuongezeka katika miaka 10 ijayo, hali hiyo huenda ikasababisha shinikizo kwa bei ya nafaka. Taarifa hiyo inasema, ongezeko la mahitaji kuhusu nishati ya mimea litasababisha kupanda kwa bei ya mazao ya kilimo. Hii italeta nafasi kwa maendeleo ya uchumi wa nchi zinazoendelea. Lakini taarifa vilevile inasema, uendelezaji wa nishati ya mimea utaleta hatari, kwanza kabisa ni kwa usalama wa nafaka. Bei kubwa ya nafaka imeathiri vibaya nchi zinazoendelea, ambazo zinakidhi mahitaji ya chakula kwa kutegemea kuagiza nafaka kutoka nchi za nje, hivyo, uamuzi wowote kuhusu nishati ya mimea unapaswa kuziangatia usalama wa nafaka pamoja na matumizi ya ardhi na maliasili ya maji.
Siku ya nafaka ya dunia ya mwaka huu imekutana na msukosuko wa mambo ya fedha duniani, msukosuko wa fedha umezidisha wasiwasi wa watu kuhusu kupanda kwa mfululizo bei ya nafaka na nishati. Katibu mkuu wa shirika la FAO, Bw. Jcques Diouf amesema ni hakika kuwa msukosuko wa fedha utaathiri uchumi wa nchi zinazoendelea hususan kilimo na usalama wa nafaka, anasisitiza, mbele ya msukosuko wa fedha, watu wasisahau msukosuko wa nafaka na kilimo.
|