Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-17 20:57:18    
Wafanyabiashara wenye asili ya China wana matumaini kubwa kuhusu maendeleo ya Asia ya Mashariki Kaskazini

cri
Mkutano wa ngazi ya juu ya wafanyabiashara wenye asili ya China duniani ambao pia ni mkutano wa baraza la ushirikiano wa uchumi wa Asia ya Kaskazini Mashariki ulifunguliwa huko Changchun mkoani Jilin. Wafanyabiashara wenye asili ya China kutoka nchi na sehemu karibu 40 duniani walikutana pamoja na kujadii fursa na njia ya ushirikiano. Watu waliohudhuria mkutano huo wana matumaini makubwa kuhusu mustakabali wa maendeleo ya Asia ya Mashariki ya Kaskazini.

Mkutano huo ni shughuli muhimu ya maonesho ya uwekezaji na biashara ya Asia ya Kaskazini Mashariki. Mikoa ya Heilongjiang, Jilin, Liaoning na Mongolia ya Ndani ya China iko katikati ya Asia ya Kaskazini Mashariki. Sehemu hiyo inapakana na Russia, Korea ya Kaskazini na Mongolia, na iko karibu na Japan na Korea ya Kusini, hivyo imekuwa kiini cha maendeleo ya ushirikiano wa kibiashara katika Asia ya Kaskazini Mashariki. Wafanyabiashara wenye asili ya China wanatilia maanani fursa hiyo. Mwenyekiti mtendaji wa shirika la wafanyabiashara wenye asili ya China duniani Bw. Kein Ting alisema, maendeleo ya uchumi wa Asia ya Kaskazini Mashariki yatakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya uchumi wa Asia katika siku za usoni, na yatawavutia wafanyabiashara wengi wenye asili ya China katika ukanda huo, akisema,

"Wafanyabiashara wa China ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi wa China. China si kama tu ni kituo muhimu cha maendeleo ya shughuli za wafanyabiashara wenye asili ya China, bali pia ni sehemu muhimu inayotiliwa maanani na nchi mbalimbali duniani wakati zinapotunga mipango ya maendeleo ya uchumi. Mwelekeo wa utandawazi wa uchumi duniani umetokea, na ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda umekuwa mwelekeo wa maendeleo ya uchumi katika karne ya 21. Nchi ya Asia ya Kusini Mashariki, China, Japan na Korea ya Kusini zitahimiza shirikiano wa kiuchumi katika Asia ya Kaskazini Mashariki, na ukanda huo utakuwa na sifa ya kipekee na maendeleo ya haraka, hasa masoko ya ukanda huo yatahimiza maendeleo ya Mongolia na sehemu ya mashariki ya Russia."

Mikoa ya Heilongjiang, Jilin na Liaoning ni kituo kikongwe cha viwanda nchini China. Katika nusu karne iliyopita, viwanda vya kemikali, chuma na chuma cha pua na magari vilianzishwa hapa, maliasili za hapa pia zimekuwa sababu muhimu ya kuwavutia wafanyabiashara wenye asili ya China. Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya sayansi ya jamii ya mkoa wa Jilin Bw. Bing Zheng alisema,

"Tukitaka kuendelea kuhimiza maendeleo ya Asia ya Kaskazini Mashariki, ni lazima tufanye shughuli mpya, na kutumia teknolojia mpya na uzoefu mpya wa usimamizi. Wafanyabiashara wenye asili ya China wana uwezo wa kufanya hivyo, na sisi hatuwezi. Lakini tunaweza kuwapatia wafanyabiashara hao fursa ya kutumia fedha, uzoefu na teknolojia zao. Kwa mfano viwanda vinavyo hitaji nguvu kazi wengi vya mikoa ya pwani ya China vinahamia mikoa ya ndani. Asia ya Kaskazini Mashariki ina fedha nyingi, nguvu kazi wengi, na miundo mbinu nzuri ikiwemo miundo mbinu ya mawasiliano. Mambo hayo yameanzisha mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wenye asili ya China kuwekeza vitega uchumi hapa. Na mambo hayo yatazinufaisha pande mbili."

Wakati mkutano huo ulipofanyika, mkuu wa shirika la wafanyabiashara wenye asili ya China nchini Marekani Bw. Tsungchin Wu aliwaalika wafanyabiashara kumi kadhaa wenye asili ya China walioko nchini Marekani kutembelea sehemu ya Kaskazini Mashariki ya China. Bw. Wu alisema hii ni mara ya pili kwake kwenda sehemu hiyo, lakini wafanyabiashara wengi walikwenda huko kwa mara ya kwanza, na hawajui mambo mengi kuhusu sehemu hiyo. Baada ya kufanya ukaguzi, wafanyabiashara hao walitambua mazingira mazuri ya uwekezaji ya huko, na wengi wao wanataka kuwekeza vitega uchumi katika shughuli mbalimbali yakiwemo mahoteli. Alisema kufanyikiwa kwa michezo ya Olimpiki ya Beijing kumewafanya wafanyabiashara wenye asili ya China wawe na imani kubwa kuhusu kuwekeza vitega uchumi katika China bara, akisema,

"Zamani wafanyabiashara wa China wanajua mambo mengi zaidi kuhusu mikoa ya Zhejiang, Jiangsu na Guangdong na mji wa Shenzhen, na hawajui mambo mengi kuhusu mikoa iliyoko kaskazini mashariki mwa China. Wengi wao walikuja hapa kwa mara ya kwanza, na wana matumani kuwa watafahamu habari nyingi zaidi. Wafanyabiashara hufanya uwekezaji katika sehemu zenye fursa nyingi. Kama mikoa ya kaskazini mashariki itawapatia fursa nzuri, bila shaka watawekeza katika mikoa hiyo."

Kwenye ufunguzi wa mkutano wa baraza la ushirikiano wa uchumi wa Asia ya Kaskazini Mashariki, mkuu wa mkoa wa Jinlin ambao ni mwenyeji wa kuandaa mkutano huo Bw. Han Changfu alisema mkoa huo unawakaribisha wafanyabiashara wenye asili ya China duniani kuwekeza vitega uchumi mkoani humo, na kushiriki kwenye kazi ya kuhimiza maendeleo ya mkoa huo na ustawi wa kituo kikongwe cha viwanda. Alisema mkoa huo utatekeleza sera ya ufunguaji mlango zaidi, kushughulikia mambo halisi, kuanzisha mazingira mazuri kwa wawekezaji, kutoa huduma bora, na kuwasiliana na kushirikiana na watu wenye asili ya China duniani kuhusu shughuli nyingi zaidi kwa karibu zaidi na ufanisi mkubwa zaidi, ili kupata mafanikio makubwa zaidi.

Kwenye mkutano huo wa wiki moja, wafanyabiashara zaidi ya mia 3 kutoka sehemu mbalimbali walishiriki kwenye majadiliano mbalimbali ya kibiashara na shughuli ya kutoa hotuba.