Kufuatia kongamano la mwisho la kugombea uchaguzi mkuu kumalizika tarehe 15 jioni, shughuli za uchaguzi mkuu nchini Marekani zimeingia katika kipindi cha mwisho kabla ya kufanyika. Katika siku zaidi ya kumi zilizosalia, mgombea urais wa Chama cha Rupublican Bw. John McCain na mgombea urais wa Chama cha Democratic Bw. Barack Obama hawatakuwa na fursa nyingine ya kutangaza ilani zao. Vyombo vya habari vinaona kuwa Bw. John McCain amekwisha shindwa, tumaini la mwisho la kubadilisha hali yake mbaya ni kuwavutia wapiga kura wanaoyumba kwenye upande wake, lakini tumaini hilo ni dogo sana.
Kongamano hilo la mwisho lilikuwa tofauti na makongamano mawili yaliyopita. Katika makongamano mawili yaliyopita, Bw. Obama na Bw. McCain walilingana katika kiasi cha uungaji mkono na hata baada ya makongamano hayo pia hawakuonekana wazi kama nani amemshinda mpinzani wake. Lakini kabla ya kongamano hilo la mwisho kufanyika, msukosuko wa fedha nchini Marekani ulimsaidia sana Obama na huku msukosuko huo umemletea pigo kubwa McCain. Gazeti la New York Times na Radio CBC hivi karibuni vilikusanya maoni ya raia, matokeo yakionesha kuwa Bw. Obama anamzidi McCain kwa 14%, kwa hiyo kongamano hilo la mwisho limekuwa fursa pekee kwa McCain kujipatia wapiga kura. Kabla ya kongamano hilo, Bw. McCain aliwaambia wapiga kura akisema, "Hivi sasa Marekani inahitaji mpiganaji jasiri, ingawa vyombo vya habari vimetoa tathmini kwamba nimeshindwa, lakini vimesahau kwamba uamuza wa mshindi ni juu yenu wala sio vyombo vya habari." Bw. Obama anajawa na uhakika na mustakbali wake wa uchaguzi, aliwaambia wapiga kura akisema "Zimebaki siku 19 tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, siku hizi 19 hazimaanishi mwisho bali ni mwanzo wa kutekeleza majukumu yangu, kazi za rais wa kipindi kijacho zitakuwa nyingi na safari ndefu."
Kuhusu kongamano hilo la mwisho watu wana hisia tofauti, baadhi wanaona kwamba ingawa McCain alishinda lakini hakuweza kubadilisha hali yake mbaya, na wengine wanaona kuwa McCain hafai lolote. Lakini jinsi Bw. Obama alivyoogombea kwa hatua madhubuti imewafanya wapiga kura wawe na imani zaidi naye. Watu wanaona kuwa baada ya kufanya makongamano mara tatu hali ya kuongoza ya Obama haikubadilika, katika muda uliosalia kama Bw. McCain akitaka kugeuza hali yake mbaya hatakuwa na chaguo lolote la kimkakati.
Kwaza, McCain hakuonekana kama ana njia yoyote ya kugeuza hali yake mbaya, kwa sababu msukosuko wa fedha unaomkwamisha hautaweza kubadilika katika muda mfupi. Pili siku chache zilizopita mashambulizi yaliyoanzishwa na McCain dhidi ya Obama kuhusu hadhi yake ya kushiriki uchaguzi mkuu yalikuwa na nia ya kugeuza uangalizi wa wapiga kura tu. Na tatu fedha za kutosha zilimwezesha Obama kununua dakika 30 za kumtangazia katika televisheni kwa siku sita mfululizo kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, lakini Bw. McCain hana uwezo huo. Bw. McCain amekubali kwamba hivi sasa shinikizo lake ni kubwa kwa sababu muda uliosalia umekuwa mfupi.
Hivi sasa McCain alichoweza kufanya ni kupunguza imani ya ukusanyaji wa maoni ya raia. Hivi karibuni matokeo ya ukusanyaji maoni ya raia yamekuwa kama sumu kwa McCain na yanaathiri vibaya wapiga kura. Vyombo vya habari vinasema, habari zilizotangazwa na gazeti la New York Times na Radio CBC haziaminiki, kwa sababu kama inavyojulikana kwa wote kwamba gazeti la New York Times siku zote linaunga mkono Chama cha Democratic, na ukusanyaji maoni ya raia ulifanyika katika eneo dogo, watu walioulizwa walikuwa 1000 tu. Katika historia, ukusanyaji maoni mara nyingi ulionesha hali ya uongo, na baadhi ya watu walioulizwa hawakusema maoni yao ya kweli. Lakini vyovyote matokeo yatakavyotokea, wakati vyombo vya habari vinapompendelea Obama, mustakbali wa uchaguzi wa uraia anaougombea McCain hautakuwa mzuri.
|