Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-20 19:30:21    
Mwimbaji wa nyimbo za kabila la Wadong bibi Wu Yuzhen

cri

Bibi Wu Yuzhen wa kabila la Wadong ni msichana mwenye umri wa miaka 23 aliyezaliwa na kuishi katika wilaya ya Liping mkoani Guiyang. Sasa yeye ni mwimbaji maarufu katika sehemu hiyo, na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa utalii wa kabila la Wadong mkoani Guizhou, kwa kuwa yeye ni hodari katika kuimba wimbo maalumu wa kabila la Wadong.

Alipokuwa mtoto, bibi Wu Yuzhen alikuwa anaishi kwa furaha, na kama watoto wengine, alianza kujifunza kuimba nyimbo za kabila la Wadong kutoka kwa waimbaji kijijini. Bibi Wu Yuzhen alisema,

"Tulijifunza kuimba nyimbo kutoka kwa wakimbaji wetu vijijini. Nyumbani kwetu kuna waimbaji wengi wanaofundisha kuimba nyimbo za kabila la Wadong, ili kurithisha utamaduani wa kabila hilo. Waimbaji wetu wa kabila la Wadong hawadai ada yoyote wanapofundisha wanafunzi, na hii ndiyo ni sababu moja ya nyimbo za kabila la Wadong kurithiwa vizuri."

Familia ya bibi Wu Yuzhen ni maskini, ili kumlipia ada ya masomo, wazazi wake wanafanya kazi za vibarua mkoani Guangdong. Bibi Wu Yuzhen alifahamu sana matatizo ya familia yake, akiwa mtoto mkubwa alikuwa anasoma masomo huku akifanya kazi za nyumbani

Mwaka 2001, bibi Wu Yuzhen alipata habari kuwa Kikundi cha Waimbaji wa Nyimbo za Kabila la Wadong cha wilaya ya Liping kilitafuta waimbaji wapya 10, akajiandikisha mara moja. Baada ya kushiriki kweye mitihani ya duru nyingi, bibi Wu Yuzhen alijitokeza kutoka kwenye washindani zaidi ya 100, na kufanikiwa kuwa mwanachama wa Kikundi cha Waimbaji wa Nyimbo za Kabila la Wadong cha wilaya ya Liping pamoja na watu wengine 9. Ili kuwafundisha vizuri wachezhaji hao wapya 10, kiongozi wa kikundi hicho aliwapeleka kusoma katika shule ya utalii ya wilaya ya Liping. Bibi Wu Yuzhen alieleza kuwa baada ya kuhitimu kwenye shule hiyo, waliweza kujiunga na vyuo vikuu. Katika miaka kadhaa aliposoma huku akifanya maonesho, bibi Wu Yuzhen alishiriki kwenye mashindano ya nyimbo za jadi za sehemu za magharibi nchini China yaliyoandaliwa na televisheni ya taifa la China, na kwenda nchi za nje kufanya maonesho. Baada ya kushiriki kwenye mashindano ya uimbaji mkoani Guizhou, bibi Wu Yuzhen aliyepata tuzo la uhodari aliandikishwa na idara ya muziki ya Chuo Kikuu cha Guizhou, kisha alichaguliwa kuwa mwakilishi wa sura ya utalii wa wilaya ya Qiandongnan. Alisema,

"Kwenye chuo kikuu, kozi yangu ni muziki wa kabila la Wadong, pia nimesoma masomo nyingine zikiwemo muziki za makabila mengine madogo madogo nchini China."

Mwezi Machi mwaka 2007 wakati maonesho ya kimataifa ya Paris ya utalii, bibi Wu Yuzhen pamoja na msichana mwingine Yang Li kwenye Kasri ya Versailles waliimba nyimbo ya kabila la Wadong kwa waheshimiwa wageni walioshiriki kwenye maonesho hayo. Nyimbo hizo ziliwavutia wakazi wengi wa Paris, ambapo nguo zao zenye umaalumu wa kabila la Wadong pia walisifiwa sana na watu wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali. Gazeti la Le Parisien la Paris lilitoa habari kuhusu maonesho ya bibi Wu Yuzhen na mwenzake kwenye sehemu muhimu ya gazeti hilo. Alipozungumzia jambo hilo lisilosahaulika, bibi Wu Yuzhen alisema,

"Kwenye maonesho hayo ya kimataifa ya utalii, China iliandaa vituo kumi kadhaa vilivyoonesha utalii wa mikoa na miji mbalimbali, na sisi tulikuwa kwenye kituo cha mkoa wa Guizhou. Watu wengi walikusanyika kwenye kituo chetu. Sisi pia tulialikwa kutoa maonesho, na watazamaji walifurahi sana, wakisema nyimbo tulizoimba ni nzuri, na nguo tulizovaa ni nzuri."

Bibi Wu Yuzhen alisema sehemu ya kabila la Wadong iko magharibi mwa China, aliona fahari kubwa kuwa nyimbo za kabila la Wadong ambazo ni sanaa yenye histori ndefu zinafuatiliwa na watu wa nchi za magharibi. Alisema Paris ni sehemu ya katikati ya sanaa na utamaduni duniani, nyimbo za kabila la Wadong zikiendelea nchini Ufarasan, zitakuwa na athari zaidi duniani."

Hivi sasa Bibi Wu Yuzhen amekuwa mwakilishi wa sanaa ya nyimbo za kabila la Wadong, na anaona kuwa ana wajibu mkubwa, alisema,

"Naona sasa wajibu wangu ni mkubwa zaidi baada ya kupata sifa nyingi, kwa kuwa siwezi kusimama tu baada ya kupata mafanikio, na ninapaswa kupata maendeleo zaidi. Sifa hizo zilipatikana kutoka watu wa nyumbani kwangu, hivyo ninafanya juhudi kadiri niwezavyo kujifunza elimu nyingi zaidi, ili kufanya mambo kwa ajili ya watu wa nyumbani kwangu, kwa vile kufanya matangazao kuhusu sehemu hiyo."

Sasa bibi Wu Yuzhen bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu, ana matumaini kuwa ataweza kutoa mchango wake kwa ajili ya urithi na uenezaji wa nyimbo za kabila la Wadong, pia ana matumaini kuwa nyimbo hizo zitafurahisha watu wote duniani. Alisema,

"Natumaini sana kuwa mtatembelea nyumbani kwangu, na kusikiliza nyimbo za kabila la Wadong, ili kujionea utamaduni wa kabila letu. Utamaduni huo ni mzuri sana."

Mwisho bibi Wu Yuzhen aliimba wimbo wa kabila la Wadong aliouimba wakati aliposhiriki kwenye mashindano ya uimbaji.