Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-20 20:25:43    
Kutembelea sehemu za peponi

cri

Wasikilizaji wapendwa, sasa tunawaletea makala ya kwanza ya Mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Vivutio vya Sichuan". Kabla ya kusoma makala hii tunatoa maswali mawili: 1, Bonde la Jiuzhaigou lilipata jina hilo kutokana na kuwepo kwa vijiji 9 vya watu wa kabila la watibet ndani ya sehemu hiyo au la? 2. Je, Bonde la Jiuzhaigou na Sehemu ya vivutio ya Huanglong zote zimeorodheshwa kuwa mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani ? Tafadhali sikilizeni kwa makini makala tunayowasomea ili muweze kupata majibu.

Bonde la Jiuzhaigou liko kwenye tarafa inayojiendesha ya makabila ya watibet na waqiang ya Aba iliyoko magharibi mwa mkoa wa Sichuan nchini China, umbo la bonde hilo ni kama lile la herufi ya Kiingereza "Y", urefu wa bonde umefikia zaidi ya kilomita 40. Kwenye bonde hilo vinatapakaa vijiji 9 vya watu wa kabila la watibet, hivyo bonde hilo limepata jina la "Jiuzhaigou", jiu, maana yake ya kichina ni 9, zhai, maana yake ni kijiji.

Bw. Nerohem Yam kutoka Israel anapenda kutembelea sehemu mbalimbali nchini China. Katika miaka kadhaa iliyopita, ametembelea miji ya Beijing na Shanghai, mikoa ya Zhejiang na Shanxi, ambapo amepata ufahamu wa kiasi fulani juu ya mila na desturi, na vivutio vya sehemu mbalimbali nchini China, lakini alipofika Bonde la Jiuzhaigou, alivutiwa sana na mandhari nzuri ya sehemu hiyo ambayo ina vivutio vyake vya kipekee. Alisema:

Bonde la Jiuzhaigou ni sehemu yenye miujiza kutokana na maji safi ya hapa. Maji hayo ni kama roho ya bonde hilo. Kwenye eneo la bonde la Jiuzhaigou, yanatapakaa maziwa makubwa na madogo zaidi ya mia moja ambayo yana rangi mbalimbali, wakazi watibet wa huko waliyaita maziwa hayo ni "Haizi" , maana yake ya kichina ni watoto wa bahari.

Maji ya maziwa hayo ni safi sana, watu wanaweza kuona waziwazi mawe madogo ya mviringo, majani na matawi ya miti yaliyokauka ndani ya maziwa hayo; na rangi ya maji ya maziwa hayo inabadilika badilika, baadhi ya sehemu maji ni ya rangi ya buluu, maji ya sehemu nyingine ni ya kijani, hata inachanganywa na rangi ya manjano. Kwa mfano, Ziwa Changhai ambalo ni ziwa kubwa zaidi kwenye Bonge la Jiuzhaiguo, ukitazama kwa karibu unaweza kuona kuwa maji ya ziwa hilo ni kijani sana, tena ni safi sana; lakini ukilitazama ziwa hilo kutoka mbali, utaona maji ya ziwa hilo ni yenye rangi ya buluu, na ziwa hilo ni tulivu ambalo halina mawimbi; ambapo vivuli vya milima ya rangi ya kijani iliyoko kando mbili za ziwa hilo vilionekana wazi kwenye ziwa, mandhari nzuri ya ziwa hilo inawapendeza sana watu.

Bw. Morishita kutoka Japan alipoona ziwa hilo linalopendeza alisifu sana akisema:

Nchini Japan, niliwahi kutazama televisheni kuhusu Bonde la Jiuzhaiguo, lakini nilipofika kwenye bonde hilo na kushuhudia mandhari nzuri namna hii, naona mandhari hiyo kweli ni nzuri zaidi kuliko niliyoona kwenye televisheni. Nchini Japana pia kuna maziwa kama hayo, lakini maziwa ya Jiuzhaigou yanapendeza zaidi.

Maji ya maziwa kwenye Bonde la Jiuzhaiguo yana rangi mbalimbali kutokana na mazingira ya asili. Bonde la Jiuzhaiguo lina umaalum wa jiolojia ya kikast, ndani ya maji ya ziwa kuna chembechembe nyingi za ion za madini ya calcium na magnesium ambazo zinaweza kuonesha mionzi ya mwanga wa rangi ya buluu na ya kijani, tena ndani ya maziwa kuna majani ya aina mbalimbali yenye rangi tofauti, ndiyo maana rangi ya maziwa inabadilikabadilika.

Maji ya maziwa kwenye Bonde la Jiuzhaiguo kwa kawaida ni ya utulivu, lakini kama maji hayo yanaweza kuporomoka kutoka kwenye miamba mirefu yenye miti, maji hayo yanaweza kuporomoka moja kwa moja kwa kasi, maporomoko ya maji yanasababisha milio mikubwa na kuwa na mandhari nzuri. Kwenye Bonde la Jiuzhaiguo, kuna sehemu 17 zenye maporomoko ya maji. Watu wakiangalia kutoka mbali, wanaweza kuona kama mapazia mengi ya maji yananing'inia kwenye mwamba mkubwa, maporomoko ya maji yanawavutia sana watu. Maporomoko yenye jina la Nourilang yamesifiwa kuwa ni mapana zaidi kuliko mengine nchini China, maji ya yanaporomoka chini kwa kufuata mwamba wenye upana wa mita zaidi ya mia moja, jinsi ilivyo kama pazima moja la maji, na chini ya mwangaza wa jua, maporomoko ya maji huonesha upinde mbalimbali wenye rangi tofauti, hali nzuri iliyoje!

Hilo ndilo Bonde la Jiuzhaiguo, ambalo linasifiwa na wachina kuwa ni sehemu ya peponi. Mwaka 1992, Bonde la Jiuzhaiguo liliwekwa na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kwenye "Orodha ya mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani".

Lakini kwa wakazi watibet wa sehemu hiyo, milima, mito, misitu na mawe kwenye bonde hilo, kila kitu kilijaliwa na mungu. Msichana wa kabila la watibet Inamanhong alisema, tangu alipokuwa mtoto alifundishwa na wazazi kuwa anapaswa kuhifadhi kwa makini zaidi kila kitu hata majani na miti kwenye Bondo la Jiuzhaiguo. Alisema:

Sisi watibet tunaamini mungu anajalia viumbe vyote duniani, na milima, mito na miti yote tulijaliwa na mungu, sisi binadamu tunapaswa kuhifadhi kila kitu na hatupaswi kukiharibu. Wazee wengi waliwaambia watoto wao wasifue nguo kwenye mito, na kutochafua maji ya mito na kila kitu cha hapa.

Msichana Inamanhong na wenzake wanaishi kwenye Bonde la Jiuzhaiguo, wote hao ni waumini wa dini ya kibudha ya Kitibet, na ni watu wenye uchangamfu na ukarimu. Watalii wakifika nyumbani kwao, wanaweza kuonja chai na vinywaji vilivyotengenezwa kwa mazao ya huko, na kutazama ngoma walizocheza watibet, na nyimbo zilizoimbwa nao, ambapo watapata furaha kubwa.

Baada ya kutembelea Bonde la Jiuzhaigou unaweza kwenda kwa gari kwenye sehemu ya Huanglong yenye vivutio na kuendelea na matembezi yako katika "sehemu nzuri kama ya peponi duniani". Sehemu ya Huanglong iko umbali wa kilomita 130 kutoka Bonde la Jiuzhaigou, sehemu ya Huanglong na Bonde la Jiuzhaigou zote zimeorodheshwa na UNESCO kwenye mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani mwaka 1992. Katika sehemu ya Huanglong, mandhari inayovutia zaidi pia ni ya maji.

Kama unataka kuangalia mandhari ya maji katika sehemu ya Huanglong unapaswa kuangalia kutoka mgongo wa mlima. Kwenye sehemu ya bonde, kuna mto unaoonekana kama dragoni ambao unapita kwenye misitu ya asili na magenge yenye theluji, na kwenye sehemu zilizopitiwa na mto kuna maziwa makubwa na madogo zaidi ya 3000 yanayoenekana kwenye mteremko wa mlima. Maziwa hayo yanang'ara chini ya mwangaza wa jua. Kati ya maziwa hayo lililo kubwa zaidi linaitwa "Ziwa lenye rangi za aina mbalimbali" ambalo limeumbika kwa maziwa madogo madogo zaidi ya 700.

Lakini kutokana na ziwa hilo liko kwenye mita zaidi ya 4000 kutoka usawa wa bahari, hakuna yeyote anayeweza kupanda. Ofisa wa Sehemu ya Huanglong Bw. Kou Yahui alisema hivi sasa wamepata njia ya kuwasaidia watalii kufika huko. Alisema,

"Mwaka huu tutajenga njia ya kebul angani, watalii wanaweza kukaa ndani ya boksi iliyosafirishwa kwenye njia hiyo ya kebul kufika huko, na pia tumekuwa tukijenga mabaa mawili ya oksijeni kuwahudumia watalii bure."

Wasikilizaji wapendwa, sasa tunatoa maswali mawili ili mjibu: 1, Bonde la Jiuzhaigou lilipata jina hilo kutokana na kuwepo kwa vijiji 9 vya watu wa kabila la watibet ndani ya sehemu hiyo au la? 2. Je, Bonde la Jiuzhaigou na Sehemu ya vivutio ya Huanglong zote zimeorodheshwa kuwa mali ya urithi wa mazingira ya asili duniani ?