Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-22 20:52:42    
Mapishi ya supu ya mboga

cri

Mahitaji:

Kuku mmoja, uyoga gramu 20, paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa gramu 20, nyanya moja, nyama ya nguruwe gramu 50, mboga gramu 50, wanga kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja

Njia:

1.osha kuku, halafu weka kwenye sufuria, mimina maji, halafu washa moto, chemsha kwa saa 3 ili kupata supu ya kuku.

2. osha mboga, kata paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa, uyoga na nyanya ziwe vipande, kata nyama ya nguruwe iwe vipande halafu changanya pamoja na chumvi, uwanga.

3. chemsha maji kwenye sufuria, halafu tia vipande vya uyoga, korogakoroga, vipakue. Tia nyama ya nguruwe kwenye maji, korogakoroga mpaka iwe na rangi ya nyeupe, ipakue.

4.mimina supu ya kuku kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia chumvi, tia vipande vya paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa, uyoga, nyanya, nyama ya nguruwe, korogakoroga, tia mboga, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.