Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-24 19:17:05    
Makampuni ya mkoa wa Jilin nchini China yatilia maanani fursa ya kuwekeza na kujiendeleza barani Afrika

cri

Maonesho ya nne ya biashara na uwekezaji ya Asia Kaskazini Mashariki hivi karibuni yalifungwa mjini Changchun, mkoani Jilin nchini China, pamoja na mkutano wa baraza la kuwekeza barani Afrika kwa makampuni ya Jilin uliohudhuriwa na maofisa wa serikali ya mkoa wa Jilin, wajumbe wa makampuni na mabalozi wa Afrika nchini China. Mwandishi wetu wa habari aliona kuwa, makampuni ya mkoa wa Jilin yanatilia maanani fursa ya kuwekeza na kujiendeleza barani Afrika na makampuni hayo yanafanya juhudi kupanua soko lao barani Afrika.

Mkoa wa Jilin ni kituo cha viwanda kilichoanzishwa miaka mingi iliyopita kaskazini mwa China na pia ni mkoa mkubwa wa kilimo, ambao una msingi mzuri wa viwanda na kilimo na maliasili nyingi. Miaka ya karibuni, wafanyabishara wa mkoa wa Jilin walijaribu kutafuta fursa ya kujiendeleza barani Afrika, kufanyika kwa wakati mmoja kwa mkutano wa Baraza la kuwekeza barani Afrika kwa makampuni ya Jilin" kutahimiza makampuni hayo kuongeza maelewano na nchi za Afrika na kuongeza madhumuni ya uwekezaji. Mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya kidiplomasia ya mkoa wa Jilin Bw. Wang Gang alisema: "shughuli zilizoanzishwa na makampuni ya mkoa wa Jilin barani Afrika zimepiga hatua ya mwanzo tu, hivyo sisi tunaitisha mkutano wa baraza hilo kwa ajili ya kutoa maarifa kwa makampuni ya mkoa wa Jilin kwenda kuwekeza barani Afrika."

Habari zinasema, tokea mwaka 2001, biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 30 kila mwaka kwa wastani. Mwaka 2005, China imekuwa rafiki mkubwa wa tatu wa biashara wa Afrika. Hivi sasa kuna makampuni 19 ya mkoa wa Jili barani Afrika na kiasi cha ujumla cha vitega uchumi kimefikia dola za kimarekani zaidi ya milioni 40. miongoni mwao, kampuni ya kimataifa ya kupeleka umeme na chansfoma ya Jilin ilishughulikia ujenzi wa miundo mbinu ya umeme nchini Sudan, Ethiopia, Guniea Ikweta na Nigeria, katika miaka ya karibuni, imeendesha biashara yake vizuri, mwaka 2007, miradi iliyojengwa na kampuni hiyo katika nchi nne za Afrika imezidi Yuan milioni 900. Katibu wa kampuni hiyo Bw. Zhang Bin ana matarajio mazuri kwa mustakabali ya maendeleo ya Afrika. Alisema: "naona soko la Afrika ni la upana. Afrika ina eneo kubwa kwa kampuni yetu kujiendeleza, hasa katika sekta ya miundo mbinu ya umeme, ambayo ni dhaifu sana. Nadhani eneo la kujiendeleza kwa hatua zaidi ni kubwa."

Kutokana na takwimu zilizotolewa na idara ya biashara ya mkoa wa Jilin, katika miezi saba iliyopita ya mwaka huu, mkoa wa Jilin uliuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 100 kwa Afrika ambayo iliongezeka kwa asilimia 46. Bidhaa zilizouzwa na mkoa wa Jilin barani Afrika ni pamoja na magari, vipuri vya gari, dawa na nguo. Mkoa wa Jilin uliagiza madini ya manganese na chromium kutoka Afrika. Pia makampuni ya mkoa wa Jili yalishiriki kwenye ujenzi wa miradi ya Afrika, kujenga madaraja, miradi ya vituo vya kupeleka umeme na chansfoma na kuzalisha umeme kwa maji.

Kutokana na kufanya kazi kwa bidii na makini, wawekezaji wa China wamepata sifa nzuri barani Afrika, nchi nyingi za Afrika zinawakaribisha wawekezaji hao kwenda kuwekeza barani Afrika. Balozi wa Ethipia Bw. Haile-Kiros Gessesse aliyetazama maonesho hayo alisema, madhumuni yake ya ziara hiyo ni kuyavutia makampuni ya mikoa iliyopo kaskazini mwa China kwenda kuwekeza nchini Ethiopia. Alisema: "makampuni mengi ya China yanazidi kuwekeza barani Afrika, hasa kuwekeza nchini Ethiopia, kwa sababu mawasiliano kati ya Ethiopia na China ni rahisi sana, kila wiki kuna safari za ndege kumi kadhaa kati ya Ethiopia na China, wawekezaji wa China ni watu wanaofanya kazi kwa makini. Waliwekeza katika sekta za utengenezaji na uchimbaji wa madini wa Ethiopia, nyingine katika sekta ya utengenezaji wa ngozi, kwa sababu idadi ya mifugo ya Ethiopia inachukua nafasi ya kwanza barani Afrika na ni nafasi ya kumi duniani, pia serikali ya Ethiopia ilitoa sera ya kusaidia, hii ni fursa zuri ya kujiendeleza.

Aidha, mkoa wa Jilin pia ulianzisha ushirikiano na nchi za Afrika katika sekta za kilimo, mpaka sasa taasisi ya ubunifu wa viwanda nyepesi ya mkoa wa Jilin imefanikiwa kuandaa semina kwa mara nane ya mafunzo ya tekenolojia ya kilimo kwa ajili ya nchi zinazoendelea, na imewafundisha mafundi zaidi 200. Mafunzo hayo ya tekenolojia ya kilimo yalihimiza uzalishaji wa chakula na utulivu wa jamii wa nchi za Afrika na kuharakisha maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi za Afrika. Mkurugenzi wa ofisi ya mawasiliano na nje ya mkoa wa Jilin Bw. Wang Gang alisema:"kilimo cha mkoa wa Jilin kina nguvu bora, mkoa huu una sifa zuri hasa katika upandaji, uzalishaji na utengenezaji wa mahindi. Chakula ni muhimu sana kwa nchi yoyote inayoendelea, pamoja na China, , na nchi nyingi za Afrika zina matatizo ya maendeleo ya uchumi na utulivu wa jamii kutokana na chakula, hivyo ushirikiano katika sekta ya kilimo ni kazi moja kubwa katika shughuli za makampuni ya mkoa wa Jilin."

Ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi ulio wa kunufaishana na nchi za Afirka umezidisha uhusiano kati ya mkoa wa Jilin na nchi za Afrika pia umeongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa China na Afrika, na unatoa mchango kwa uhusiano wa kiwenzi kati ya China na Afrika.