Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-27 18:47:53    
Waziri mkuu wa Kazakhstan ahojiwa na waandishi wa habari wa China

cri
Kabla ya kufunga safari kwa waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kuelekea Kazakhstankwa ziara rasmi na kuhudhuria mkutano wa 7 wa mawaziri wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai, waziri mkuu wa KazakhstanBw. Karim Masimov alihojiwa na waandishi wa habari wa China akiwemo wa Radio China Kiamtaifa, ambapo akizungumzia uhusiano kati ya China na Kazakhstanalisema, hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kiwango cha juu sana cha maendeleo. Alisema:

"Rais Nazarbayev wa Kaskstan amedhihirisha wazi kuwa, China ni mwenzi wa kimkakati wa Kasakstan, China ina umuhimu wa kimkakati katika sera ya Kazakhstanjuu ya uhusiano na nchi za nje. Nchi zetu mbili zina maoni ya pamoja kuhusu masuala makubwa ya Kimataifa, na tuna matumaini kuwa uhusiano kati ya nchi zetu mbili utadumisha mwelekeo wa maendeleo ya kiwango cha juu.

Bw. Masimov alisema, ziara ya waziri mkuu wa China Bw. Wen Jibao nchini Kazakhstanitafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, hii itakuwa ziara muhimu inayohusu mambo mengi, ambayo itahimiza juhudi za kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Kazakhstanitafikia dola za kimarekani bilioni 10, na mwishoni mwa mwaka huu lengo lililotolewa na marais wa nchi hizo mbili kuhusu kuongeza thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili iongezeke na kufikia dola za kimarekani bilioni 20 linatazamiwa kutimizwa. Bw. Masimov alisema:

Miundo ya kiuchumi ya China na Kaskastan inaweza kusaidiana, na pande hizo mbili zina nguvu kubwa ya kujiendeleza katika mambo ya uchumi. Tunatakiwa kuongeza thamani ya biashara kati yetu, kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu kwenye sehemu za mipakani ili kuongeza uwezo wa biashara kwenye sehemu hizo. Kazakhstaninavutia vitega uchumi vya China, pia inataka makampuni ya China yaende Kazakhstankuwekeza vitega uchumi, naona pande mbili zina nguvu kubwa ya kufanya ushirikiano katika sekta hiyo.

Bw. Masimov alifahamisha kuwa, katika kazi ya kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, Kazakhstanimeiga maarifa iliyopata China katika miaka 20 hadi 30 iliyopita. Alisema:

Tunaona kuwa, hivi sasa msukosuko wa fedha uliotokana na msukosuko wa mikopo ya ngazi ya pili nchini Marekani ni msukosuko mkubwa zaidi wa fedha katika miaka 30 iliyopita. Matokeo yake yataleta athari ya muda mrefu kwa nchi mbalimbali zilizoko katika mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani, ambapo nchi yoyote inatakiwa kukabiliana na msukosuko huo. Katika hali hiyo, ushirikiano kati ya Kazakhstanna China utaonesha umuhimu wake mkubwa zaidi.

Alipozungumzia maendeleo ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai, Bw. Masimov alisema:

Naona Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai iliyoanzishwa kwenye msingi wa kutatua masuala ya mipaka imendelezwa kuwa jumuia kubwa ya ushirikiano, ambayo ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za aina mbalimbali duniani. Makubaliano mengi yaliyosainiwa na marais wa nchi na viongozi wa serikali za nchi wanachama wa jumuia hiyo kuhusu usalama wa dunia, usalama wa chakula, na masuala ya uchumi yatakuwa na umuhimu mkubwa, Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai itakuwa jumuia muhimu ya kukabilina na changamoto zinazoikabili dunia nzima.

Bw. Masimov alidhihirisha kuwa, nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai zinapaswa kuongeza ushirikiano katika sekta ya uchumi.