Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-29 16:50:22    
China yaanza kujenga kituo cha tatu cha utafiti kwenye ncha ya kusini ya dunia ya dunia

cri

Kikundi cha 25 cha kufanya utafiti kwenye ncha ya kusini ya dunia cha China hivi sasa kimefunga safari. Watafiti wa kikundi hicho watakamilisha ujenzi wa kituo cha tatu cha utafiti wa kisayansi Kunlun kwenye ncha ya kusini ya dunia ndani ya muda wa nusu mwaka. Kituo hicho pia ni kituo cha kwanza cha China kwenye sehemu ya ndani ya ncha ya kusini ya dunia ya dunia. Imefahamika kuwa ujenzi wa kituo hicho ni alama kuwa shughuli za utafiti wa China kwenye ncha ya kusini ya dunia ya dunia zimepanua kutoka sehemu ya mpaka wa ncha hiyo hadi kufikia sehemu ya katikati ya ncha hiyo.

Hivi sasa ingawa nchi 28 duniani zimejenga vituo 53 vya utafiti wa kisayansi kwenye ncha ya kusini ya dunia, lakini vingi vyao viko kwenye sehemu za mpakani mwa ncha hiyo, nchi sita tu duniani zikiwemo Marekani, Russia na Japan zilijenga vituo vya utafiti wa kisayansi kwenye sehemu ya katikati ya ncha ya kusini ya dunia ya dunia. Msemaji wa idara ya bahari ya China Bw. Li Haiqing alisema, kituo hicho kitakachojengwa China kiko kwenye sehemu ya mwinuko wa barafu, ambacho kiko juu zaidi kuliko vituo vya nchi mbalimbali kwenye ncha ya kusini ya dunia.

Kujenga kituo hicho kwenye sehemu ya mwinuko wa barafu ni uamuzi ulifanywa baada ya kufanya utafiti wa mambo mbalimbali. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti kwenye ncha za dunia katika idara ya bahari ya China Bw. Qu Tanzhou alisema, kwanza sehemu hiyo inafunikwa na barafu yenye kina kikubwa. Pili data kuhusu mzingira ya dunia katika miaka zaidi ya milioni moja iliyopita zitapatikana kwa kuchimba chini ya barafu kwenye sehemu hiyo, na data hizo zitasaidia kufuhamu kanuni za mabadiliko ya mazingira ya dunia na suala la mabadiliko ya hali ya hewa linalofuatiliwa duniani. Bw. Qu Tanzhou alisema:

"kazi za uchimbaji wa barafu haziwezi kumalizika katika muda mfupi, kwa hiyo kazi hizo lazima ziungwe mkono na kituo cha utafiti, data muhimu na zenye thamani kubwa zitapatikana tu baada ya kuchimba kwa muda mrefu na mfululizo."

Aidha sehemu ya mwinuko A ya barafu kwenye ncha ya kusini ya dunia ni sehemu nzuri kabisa duniani ya kufanya utafiti wa unajimu, matokeo yake yanafanana na yale ya utafiti kwenye kituo kilichoko kwenye anga ya juu.

Imefahamika kuwa, kituo cha Kunlun chenye eneo le mita za mraba zaidi ya mia tano kitakuwa na vifaa ya kuzalisha umeme, kushughulikia maji, mawasiliano na upashanaji habari, na kitaweza kukidhi mahitaji ya kazi na maisha ya watafiti 24.

Mkurugenzi wa ofisi ya barafu katika kituo cha utafiti wa ncha za dunia cha China Bw. Li Yuansheng pia ni kiongozi cha timu ya utafiti wa barafu kwenye ardhi ya ndani ya kikundi hicho cha utafiti wa ncha ya kusini ya dunia. Alisema, ili kukabiliana na halijoto ya chini kwenye sehemu ya ardhi ya ndani ya ncha ya kusini ya dunia, kituo cha Kunlun kitajengwa kwa kutumia muundo maalum wa chuma cha pua. Bw. Li Yuansheng alisema:

"sehemu ya barafu ya ncha ya kusini ya dunia inafunikwa na theluji yenye kina cha mita mia moja. data zilizotumwa na kituo cha utafiti wa hali ya hewa cha huko zimeonesha kuwa halijoto ya chini kabisa inaweza kufikia nyuzi 82 chini ya sifuri, kwa hiyo vifaa vitakayotumika katika ujenzi wa kituo hicho lazima viweze kuhimili baridi ya namna hii."

Imefahamika kuwa muundo mkuu wa kituo hicho utajengwa kwa kutumia chuma maalum cha pua, na vifaa na vipuri 21 vitakayotumika vyote vilifanywa majaribio kwenye hali ya baridi kali, ili kuhakiksha kuwa vitafanya kazi kama kawaida kwenye mazingira ya ncha ya kusini ya dunia.

Kabla ya hapo, China ilijenga vituo viwili vya utafiti vya Changcheng na Zhongshan mwaka 1985 na 1989 kwenye sehemu ya mpakani ya ncha ya kusini ya dunia. Baada ya kituo cha Changcheng kumalizika kujengwa, China inafanya shughuli za utafiti wa kisayansi kwenye ncha ya kusini ya dunia kila mwaka, na China imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa hali ya hewa, barafu, viumbe, kemikali na fiziki ya baharini kwenye ncha ya kusini ya dunia.

Kikundi cha 25 cha utafiti wa ncha ya kusini ya dunia kinachobeba jukumu wa kujenga kituo cha Kunlun kinaundwa na watu 204, ambao ni wengi zaidi kuliko shughuli zote za utafiti zilizopita. Kikundi hicho kilifunga safari tarehe 20 mwezi huu kutoka mjini Shanghai na kuelekea ncha ya kusini ya dunia.

Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa ncha za dunia katika idara ya bahari ya China Bw. Qu Tanzhou alisema, baada ya maendeleo ya miaka mingi, hivi sasa China imekuwa na uwezo wa kufanya utafiti wa kisayansi kwenye eneo la ardhi ya ndani la ncha ya kusini ya dunia. Lakini watafiti wa kikundi hicho bado watakabiliana na matatzio mbalimbali katika ujenzi wa kituo cha Kunlun. Bw. Qu Tanzhou alisema:

"tatizo kubwa kwenye sehemu hii ni baridi kali na upungufu wa Oxygen, kituo cha Kunlun kitajengwa kwenye sehemu ya mwinuko yenye urefu wa mita elfu nne, ambayo mazingira yake yanafanana na yale ya sehemu yenye urefu wa mita elfu 5 kutoka usawa wa bahari nchini China, kiwango cha Oxygen kwenye hewa ni cha chini sana."

Watafiti wote wa kikundi hicho walipita kwenye upimaji mbalimbali mkali wa afya, saikolojia na mazoezi ya kwenye mazingira ya nje. Bw. Qu Tanzhou alisema, katika safari hii, watamaliza kazi za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi na vya kufanya utafiti vyenye uzito wa zaidi ya tani 600. Bw. Qu Tanzhou alisema:

"kikundi hicho kitasafirisha vifaa vingi sana, tutaunda msafara wa magari 12 maalum yanayosafiri kwenye theluji na kumaliza kazi za kusafirisha vifaa vya ujenzi na vya kufanyia utafiti vyenye uzito wa zaidi ya tanni 600."

Bw. Qu Tanzhou alijulisha kuwa, kutokana na mpango uliowekwa, ujenzi wa kituo cha Kunlun utamalizika mwezi Januari mwaka kesho. Mwanzoni kituo hicho kitafanya kazi katika majira ya joto tu, katika miaka kadhaa ijayo, China itafanya juhudi kukamilisha ujenzi wa kituo hicho na kukiwezesha kifanye kazi mwaka mzima.