Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-07 15:54:47    
Wachina wanaoishi nchini Zimbabwe wafuatilia wagonjwa wa Ukimwi wa huko

cri

Mfanyabiashara wa China Bw. Xie Chonghui ambaye anaitwa na wakazi wa huko kuwa "mfalme wa baiskeli", alasiri ya tarehe 10 Oktoba akiendesha lori lililobeba mikate alikwenda kituo cha kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi kilichoko kitongoji cha mji wa Harare. Alifika kwenye kituo hicho akifuatana na balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Yuan Nansheng, ambapo mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Mcallen na wafanyakazi wengine waliwakaribisha kwa furaha.

Bi. Mcallen nwenye umri wa miaka zaidi ya 70 alimwambia Bw. Yuan Nansheng kuwa, " Hii ni kazi kubwa, tunawakaribisha wachina kushiriki kwenye shughuli za kuwaokoa na kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi." Bi. Mcallen alikwenda Zimbabwe mwaka 1983 akiwa mmoja kati ya watu wanaojitolea, na kuanzisha mwenyewe kituo hicho cha kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi kinachoweza kupokea wagonjwa zaidi ya 6,000.

Wako wagonjwa wengi wa Ukimwi nchini Zimbabwe, ambao wanafuatiliwa na wachina wanaoishi nchini Zimbabwe. Ubalozi wa China nchini Zimbabwe mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu ulianzisha shughuli za wafanyabiashra wa China kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi, yatima na walemavu zilizoshirikisha mashirika ya China na kampuni za China nchini Zimbabwe. Katika miezi miwili iliyopita, kampuni za China na wafanyabiashara wa China waliwapa vifaa vingi wagonjwa wa Ukimwi. shughuli hizo zilisifiwa na serikali na wakazi wa huko, na vyombo vya habari vya huko vilitangaza shughuli hizo na kuzisifu sana.

Bw. Yuan Nansheng alisema, shughuli hizo ni mahitaji ya kutekeleza moyo wa mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka 2006, ni mahitaji ya kutekeleza majukumu ya kijamii na kutimiza maendeleo ya muda mrefu.Kwa kampuni za China katika nchi za nje, pia ni mahitaji ya hali halisi ya Zimbabwe. Shughuli hizo zina umuhimu mkubwa kwa kuboresha na kuimarisha msingi wa kiraia wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kuinua sura ya wachina wanaoishi nchini Zimbabwe. Baada ya muda wa miezi miwili tu, shughuli hizo zimepata maendeleo.

Hivi sasa hali ya uchumi nchini Zimbabwe inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, kutokana na sababu ya kisiasa, misaada iliyotolewa na mashirika ya kuwahudumia wagonjwa wa Ukimwi ya nchi za nje bado haijapatikana, na wagonjwa wengi wa Ukimwi wa huko walikosa dawa na vyakula. Wakati balozi Yuan Nansheng na Bw. Xie Chonghui walipokabidhi mikate mikononi mwa wagonjwa hao, wengi wao walitokwa na machozi.

Kampuni saba za China nchini Zimbabwe zilitoa vyakula na nguo kila baada ya muda fulani kwa kituo hicho cha kuwafuatilia wagonjwa wa Ukimwi, baadhi ya wachina wanaoishi nchini Zimbabwe pia wametunza yatima 15 wa Ukimwi. Kampuni kadhaa za China si kama tu ziliajiri wagonjwa wa Ukimwi wa huko, bali pia ziliwapa mshahara watu wasioweza kufanya kazi kutokana na ugonjwa wa Ukimwi. Baada ya wagonjwa kufariki, kampuni hizo pia zilitoa ruzuku kwa jamaa zao.

Imefahamika kuwa wachina wengi nchini Zimbabwe walitoa vifaa vingi kwa shule na mashirika ya huruma ya huko katika muda mrefu uliopita, na kujenga uhusiano mzuri wa ushirikiano na mashirika hayo. Shughuli za huruma zilizofanywa na wachina ziliwafanya wakazi wa huko waelewe kampuni za China, na kuonesha umuhimu mkubwa katika kujenga uso wa China na wa kampuni za China.

Bw. Xie Chonghui ambaye alikwenda barani Afrika katika miaka ya 90 ya karne iliyopita alisema, inapaswa kuhudumia jamii wakati wa kufanya biashara, kama hakuna maelewano na misaada ya wakazi wa huko, hawezi kupata mafanikio kwenya biashara. Alieleza kuwa wafanyabiashara wa China nchini Zimbabwe wanapaswa kushikilia kuhudumia jamii za huko.

***************************

Habari nyingine zinasema, wafanyabiashara zaidi ya 400 kutoka Kenya walishiriki kwenye maonesho ya 104 ya bidhaa zinazosafirishwa nje na zinazoagizwa kutoka nje ya China yaliyofungwa hivi karibuni huko Guangzhou. Habari zinasema kutokana na kuathiriwa na msukosuko wa fedha na kupungua kwa ongezeko la uchumi duniani, idadi ya jumla ya watu walioshiriki kwenye maonesho hayo ilipungua, lakini idadi ya wafanyabiashara wa Kenya walioshiriki kwenye maonesho hayo iliongezeka na kuweka rekodi katika historia ya nchi hiyo.

Hivi sasa ongezeko la uchumi wa dunia linapungua, lakini kampuni nyingi za Kenya zinapanga uwekezaji mpya, ambazo zinataka kuagiza vifaa na zana mpya ili kupunguza gharama.

Wafanyabiashara wengi wa Kenya walisema, vifaa na zana nyingi zinazouzwa na kampuni za Ulaya na Marekani zinatumika katika viwanda vikubwa. Kwenye maonesho hayo yaliyofanyika huko Guangzhou, wanaweza kuagiza zana zinazofaa kwa viwanda vidogo na vya ukubwa wa kati hata karakana, na bidhaa hizo zinawavutia wafanyabiashara wa Kenya.

*******************************

Kongamano la uhusiano kati ya China na Afrika na dunia ya hivi leo lililoendeshwa na taasisi ya historia ya Afrika ya China na chuo cha historia na utamaduni cha chuo kikuu cha Shanxi lilifanyika hivi karibuni mjini Taiyuan mkoani Shanxi, China.

Wajumbe waliohudhuria kongamano hilo waliona kuwa, katika miaka kadhaa iliyopita, hasa tangu mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulipofanyika hapa Beijing, uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika si kama tu ulidumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, bali pia ulinufaisha pande mbili za China na Afrika katika pande nyingi.

Wasomi wengi waliohudhuria kongamano hilo waliona kuwa, maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika yalionesha umuhimu wa kuigwa, nchi nyingi, mashirika ya kimataifa na kampuni nyingi zilieleza kuwa zinapenda kushiriki kwenye miradi ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2008-11-07