Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-03 19:41:16    
Wu Bangguo kutembelea nchi 5 za Afrika

cri

Kutokana na mwaliko wa viongozi wa mabunge ya nchi 5 za Algeria, Gabon, Ethiopia, Madagasca na Seychelles, spika wa bunge la China, Bw. Wu Bangguo atafanya ziara rasmi ya kirafiki katika nchi hizo kuanzia tarehe 3 mwezi huu, tena ataitembelea kamati ya Umoja wa Nchi za Afrika, ambao makao makuu yake yako Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. Naibu spika wa bunge la umma la China, Bw. Cao Weizhou alisema, ziara hiyo ya Bw. Wu Bangguo hakika itaimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi hizo, Bw. Cao alisema,

"Bunge ni idara ya utungaji sheria ya ngazi ya juu zaidi katika kila nchi, ambalo linaonesha madai ya wananchi, kuimarisha maingiliano na ushirikiano wa idara za utungaji sheria, kunaimarisha maelewano na kuaminiana kati yao. Kila bunge kujifunza kutoka kwa uzoefu wa bunge la nchi nyingine ni muhimu sana katika kukuza uhusiano wa pande mbili, alisema bunge la China linataka kuimarisha maingiliano na mabunge ya nchi hizi tano katika ngazi mbalimbali na kujadili ushirikiano wa pande nyingi kati ya bunge la China na mabunge ya nchi za Afrika."

Shughuli rasmi za matembezi ya Bw. Wu Bangguo katika nchi 5 za Afrika zitaanza tarehe 4 mwezi Novemba, ambayo ni siku ya kufunguliwa kwa mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano la China na Afrika miaka miwili iliyopita. Kwenye mkutano huo, viongozi wa China na Afrika walikubaliana kujenga uhusiano mpya wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Afrika, ambao ni wa usawa, kuaminiana na kunufaishana katika ushirikiano wa kiuchumi na maingiliano ya kiutamaduni. Katika siku ya kutimiza miaka miwili tangu ufanyike mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika, Bw. Wu Bangguo anaitembelea tena Afrika, mkurugenzi wa idara ya Afrika ya wizara ya mambo ya nje ya China, Bi. Xu Jinghu alisema, kufanya ziara ya kirafiki sasa katika nchi za Afrika kwa Bw. Wu Bangguo, kunachangia uimarishaji wa uhusiano kati ya China na Afrika. Bi Xu alisema,

"Mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika ulifanyika mwaka 2006, mwaka huu ni mwaka wa pili wa kutekeleza maazimio ya mkutano huo, ambao ni muhimu zaidi kwa kuimarisha mafanikio ya mkutano, ziara ya Bw. Wu Bangguo licha ya kuimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi hizo 5, pia itafanya kazi muhimu kwa uendelezaji wa uhusiano mpya wa kiwenzi na kimkakati uliothibitishwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi, na kutekeleza vizuri maazimio yaliyopitishwa mkutanoni."

Kabla ya miaka miwili iliyopita, rais Hu Jintano wa China alitangaza mkutanoni hatua 8 za kuyaunga mkono maendeleo ya nchi za Afrika, ambayo moja ya hatua hizo ni China kutoa msaada wa kujenga kituo cha mikutano cha Umoja wa Afrika. Katika ziara yake hiyo, Bw. Wu Bangguo atatembelea Adis Ababa, na kushiriki sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho cha mikutano, Bi. Xu Jinghu alisema,

"Ujenzi wa kituo cha mikutano cha Umoja wa Afrika ni mradi wa ujenzi wa utoaji msaada wa China unaochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa hivi sasa baada ya mradi wa ujenzi wa njia ya reli ya TAZARA, spika wa bunge la China, Bw. Wu Bangguo atashiriki sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo, ambacho ujenzi wake utakamilishwa mwaka 2010."

China inatarajia ziara hiyo ya Bw. Wu Bangguo iweze kuimarisha uratibu na ushirikiano wa China na nchi hizo tano pamoja na Umoja wa Afrika katika mambo ya kimataifa, kuharakisha ujenzi wa miradi ya utoaji misaada, na kuimarisha ushirikiano na nchi hizi tano katika ujenzi wa miundo-mbinu, uendelezaji na matumizi ya rasilimali, mafunzo ya kazi, kilimo na utalii kwa kufuata kanuni za kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, mbali na hayo, inaendelea kuhimiza viwanda vya China viwekeze katika nchi hizo tano.