Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-05 18:28:04    
Tianjin yaharakisha shughuli za kuendeleza dawa za jadi za kichina

cri

Kutia maji kwenye mchanganyiko wa dawa za mitishamba na kuchemsha kwa muda mrefu kwenye chungu la kauri, maji yenye rangi nzito yanapatikana baada ya kuchuja supu ya mitishamba hiyo. Wachina wanayaita maji hayo "supu ya dawa", na walizoea kutumia supu ya namna hiyo kutibu magonjwa mbalimbali. Hivi sasa watafiti wa China wanajitahidi kutumia teknolojia za kisasa kwa kubadilisha ustadi huo wa jadi uliotumika kwa miaka mingi, yaani kuchuja moja kwa moja vitu muhimu kutoka kwenye mitishamba hiyo na kuitengeneza kuwa vidonge au dawa ya sindano, si kama tu inarahisisha utumiaji wa dawa hizo bali pia ufanisi wake umeimarika zaidi. Mji wa Tianjin ulioko kaskazini mwa China umefanya juhudi katika eneo hilo na umepata maendeleo dhahiri.

Kundi la Tasly lililoanzishwa mwaka 1994 hivi sasa limekuwa moja ya makampuni makubwa ya dawa za jadi za kichina mjini Tianjin. Dawa moja ya kutibu magonjwa ya moyo inayozalishwa na kundi hilo inaleta pato la yuan bilioni kadhaa nchini China kila mwaka. Dawa hiyo pia inatazamiwa kupata uthibitisho wa idara ya usimamizi wa chakula na dawa ya Marekani. Mkurugenzi wa bodi ya kundi la Tasly Bw. Yan Xijun alisema,

"baada ya juhudi za miaka zaidi ya 10 za kuendeleza dawa za jadi za kichina, hivi sasa tunaiendeleza zaidi dawa hiyo kwa uvumbuzi, tumeanzisha mfumo wa uvumbuzi wa dawa hiyo, pia tunachukua vitu muhimu kwenye mitishamba na na kuanzisha database maalum, na tunaweza kuvumbua dawa nyingi mpya kutokana na mfumo huo."

Kundi la dawa l Zhongxin la Tianjin ni moja ya makampuni yanayotangulia katika kuziendeleza dawa za jadi za kichina. Tofauti na kundi la Tasly, kundi hilo ni kundi la makampuni mengi ya chapa maarufu ya dawa nchini China yakiwemo Tongrentang, Darentang na Longshunrong. Chapa hizo zina historia ndefu na zinajulikana kote duniani, lakini makampuni hayo hayakusita mbele ya mafanikio ya zamani, bali yameendelea kufanya juhudi katika mageuzi ya mfumo wa kanuni za dawa na utafiti wa teknolojia mpya za dawa za jadi za kichina. Naibu maneja mkuu wa kundi hilo Bw. Zhang Qiang alisema:

"tuna mkakati wetu, na tunalenga kuunda nguvu yetu ya ushindani katika soko la nchini China na duniani kwa kutengeneza dawa mpya, kutumia teknolojia mpya na kuanzisha soko jipya."

Imefahamika kuwa, kundi la Zhongxin hivi sasa linazalisha aina zaidi ya 500 za dawa, baadhi ya dawa hizo zitauzwa kwa nchi na sehemu zaidi ya 20 duniani zikiwemo Japan, Russia na Marekani.

Dawa za jadi za kichina ni moja ya uridhi muhimu wa utamaduni wa miaka ya elfu tano ya China, kwa muda mrefu uliopita ufanisi wake dhahiri wa kimatibabu umehakikisha ustawi wa taifa la China. ili kueneza dawa hizo duniani na kunufaisha binadamu wote, katika miaka ya hivi karibuni serikali ya China imechukua hatua mbalimbali kufanya uzalishaji wa dawa za kichina ufuate njia za kisayansi na kanuni husika. Mji wa Tianjin ulithibitishwa na serikali miaka mitatu iliyopita kuwa kituo cha sayansi na teknolojia za kisasa za dawa za kichina.

Hivi sasa mji wa Tianjin umekuwa na sekta kubwa ya kisasa ya kutengeneza dawa za jadi za kichina inayoundwa na makundi mawili ya Tasly na Zhongxin, pia mji huo ulijenga maabara ya taifa ya dawa, kituo cha utafiti wa dawa mpya cha Tianjin, kituo cha uhandisi wa teknolojia za kisasa za dawa za kichina na kituo cha upimaji wa sifa ya dawa za kichina.

Aidha, Tianjin pia umepata maendeleo mengi katika utafiti wa teknolojia muhimu za dawa za kichina, tekonolojia zaidi ya 20 muhimu zikiwemo teknolojia ya membrane na nanometer zimetumika katika uzalishaji wa dawa hizo.

Imefahamika kuwa, hivi sasa Tianjin inazalisha aina 800 za dawa za jadi za kichina zilizopata idhini kutoka kwa serikali, inaweza kuzalisha dawa za aina 26 tofauti zikiwemo vidonge na sindano, zaidi ya 200 za dawa hizo ziliandikishwa na kuuzwa nje ya China. ingawa hivyo shughuli za kuendeleza dawa za jadi za kichina bado zimepiga hatua za mwanzo tu mjini Tianjin na hata nchini China. ofisa mhusika wa serikali ya Tianjin Bi. Zhou Hong alisema:

"lengo la kituo cha kuendeleza dawa za kichina cha Tianjin ni kuimarisha usambazaji wa dawa, upashanaji habari husika na utafiti wa teknolojia za dawa, pia tunalenga kuharakisha maendeleo ya dawa za jadi za kichina, kupanua soko la kimataifa, kuvumbua aina mpya za dawa za jadi za kichina, na kuandaa makundi ya kutengeneza dawa yenye uwezo mkubwa wa uvumbuzi."

Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, Tianjin itakamilisha mfumo wa uvumbuzi wa dawa za jadi za kichina ifikapo mwaka 2010, kujenga vituo 50 vya kupanda mitishamba, na aina mbili za dawa hizo zitaingia kwenye soko la kimataifa, mji wa Tianjin utakuwa kituo kikubwa cha dawa za kichina chenye uwezo wa jumla wa uzalishaji, upashanaji habari na uuzaji wa dawa kwa nje.

Kutokana na mpango huo, makampuni mengi ya dawa mjini Tianjin yameweka mkazo katika utafiti wa dawa za kisasa za kichina. Kundi la Tasly pia lina mpango wake. mkurugenzi wa bodi wa kundi hiyo Bw. Yan Xijun alisema:

"tutaweka mkazo katika kazi za utafiti na kuimarisha zaidi msingi wa sekta yetu, tunalenga kunufaisha China na dunia nzima kwa dawa zetu mpya zenye hakimiliki, zenye teknolojia ya juu, ufanisi mzuri na sifa ya kuaminika."