Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-06 20:08:37    
Medvedev atoa taarifa kuhusu mambo ya taifa

cri

Rais Dimitri Medvedev wa Russia tarehe 5 alitoa taarifa kuhusu mambo ya taifa kwa mabaraza mawili ya bunge la shirikisho la Russia. Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kutoa taarifa kuhusu mambo ya taifa kwa bunge la taifa tangu achaguliwe kuwa rais, ambayo pia ni taarifa ya 15 kuhusu mambo ya taifa iliyotolewa na rais wa nchi hiyo. Katika mazingira ambayo uhusiano kati ya Russia na nchi za magharibi umezorota tangu kuzuka mapigano kati ya Russia na Georgia mwaka huu na kuzidi kuwa mbaya kwa msukosuko wa fedha duniani, taarifa iliyotolewa safari hii na rais Medvedev inafuatiliwa zaidi na watu.

Kwa kufuata maagizo ya katiba ya shirikisho la Russia, rais wa Russia kila mwaka anatakiwa kutoa taarifa kwa bunge la taifa kuhusu hali ya nchini na sera za ndani na kwa nje. Kwa kawaida shughuli hizo zinafanyika kila mwaka kwenye ukumbi wa marmar wa kasri ya Kremlin. Lakini mwaka huu rais Medvedev hakufuata desturi hiyo, bali alichagua ukumbi wa Georgi, ambao ulitumika kufanyia sherehe ya kuapishwa kwake kushika wadhifa wa urais. Wajumbe zaidi ya 800 wakiwa ni pamoja na waziri mkuu Putin, spika wa baraza la juu la bunge, Bw. Mironov, spika wa baraza la chini la bunge, Bw. Leiziluofu, walisikiliza taarifa hiyo.

Msukosuko wa fedha na hali ya kimataifa baada kuzuka kwa mapambano kati ya Russia na Georgia, ambayo yanafuatiliwa sana na watu duniani, pia ni masuala yaliyotiliwa mkazo kuelezwa.

Kuhusu msukosuko wa fedha unaoendelea hivi sasa, Bw. Medvedev katika taarifa yake hiyo alisema, yanapaswa kufanywa mageuzi kuhusu utaratibu wa kisiasa na kiuchumi uliopo hivi sasa duniani. Russia itapitisha sheria za kujenga kituo cha mambo ya fedha cha kimataifa nchini Russia. Alidai pia kufanya hesabu ya urali katika biashara ya mafuta ya petroli na gesi ya asili kwa fedha ya Rubles. Alisema, Russia itaondolea mbali athari za msukosuko wa uchumi wa kimataifa na kuimarika zaidi.

Kuhusu mapigano yaliyozuka kati ya Russia na Georgia mwezi Agosti mwaka huu, Bw. Medvedev alishutumu Marekani na jumuiya ya NATO kwa kutumia vigezo viwili kuhusu masuala ya Kosovo na Ossetia ya Kusini, alizilaumu Marekani na NATO kujipanua kwa upande wa mashariki na kupanga mfumo wa kutungulia makombora kwenye Ulaya ya mashariki.

Alisema, Russia itazikabili kwa kuchukua hatua za mwafaka. Alisema, Russia itapanga makombora ya aina ya "Iskander" katika jimbo la Kaliningradskaya obl ili kuikabili Marekani kupanga mfumo wa kutungulia makombora katika Ulaya ya mashariki. Mbali na hayo, Bw. Medvedev alisema, inapaswa kuchukua hatua mbalimbali halisi kuimarisha usalama wa dunia, na kuimarisha msingi wa sheria kuhusu uhusiano wa kimataifa; na ni lazima kujenga utaratibu wa uhusiano wa kimataifa wenye vitovu vingi, dunia haiwezi kudhibitiwa na nchi moja tu. Alisisitiza, wakati wa kujenga mfumo mpya wa usalama wa pamoja duniani umefika zamani. Russia itaanzisha mazungumzo na Ulaya kuhusu suala la usalama.

Alipozungumzia uhusiano wa Russia na Marekani, Bw. Medvedev alisema, anatarajia rais mteule wa Marekani atafanya uamuzi wa kuimarisha uhusiano na Russia. Alisema, Russia haina matatizo juu ya watu wa Marekani, wala haina wazo la kuipinga Marekani. Russia inatarajia serikali mpya ya Marekani, ambayo ni mwenzi wa Russia, itafanya uamuzi wa kuimarisha uhusiano na Russia.

Bw. Medvedev katika taarifa hiyo alieleza kwa kirefu kuhusu ufisadi. Alisema, ufisadi ni adui mkubwa wa taifa, inatakiwa kufanya kwa makini kazi za kupinga ufisadi kwa kuchukua hatua za tahadhari ikiwemo ya kujenga utaratibu mkali wa usimamizi wa mali ya taifa.

Taarifa hiyo ilisomwa kwa karibu dakika 90, Bw. Medvedev alieleza maoni yake kuhusu ujenzi wa utaratibu wa sheria za nchi, ujenzi wa jeshi, uhusiano kati ya serikali za shirikisho na za mitaa, mambo ya utamaduni, elimu na afya pamoja na huduma za jamii.