
China imeonesha rasmi picha ya kwanza ya sura nzima ya sayari ya mwezi, ambayo imetengenezwa kwa mujibu wa picha zilizopigwa na satelaiti ya Chang'e No.1 ya kuchunguza sayari ya mwezi iliyorushwa na China mwaka 2007.
Imefahamika kuwa, picha hiyo ni picha yenye sura ya mwezi iliyo kamili zaidi kuliko picha nyingine zilizowahi kuoneshwa duniani.
Wanasayansi wa China wamesema, hivi sasa satelaiti hiyo ya Chang'e No.1 inafanya kazi vizuri, kwa hiyo wameamua kuendelea kufanya majaribio mengine ya kisayansi ili kulimbikiza data na uzoefu kwa ajili ya utafiti wa siku zijazo. Mbali na hayo China inatazamiwa kurusha satelaiti ya pili ya utafiti wa sayansi ya mwezi kabla ya mwishoni mwa mwaka 2011.
|