Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-14 16:19:09    
Daktari wa China atoa mchango mkubwa kwa miaka 40 nchini Mali

cri

Tokea mwaka 1968, madaktari wa China walikwenda Mali kushughulikia matibabu na afya za wananchi wa Mali. Mwaka huu ni wa 40 tangu China itoe msaada wa matibabu kwa Mali. Katika miaka 40 iliyopita, kikundi cha madaktari wa China kiliwaokoa na kuwatibu wananchi wa Mali na kusifiwa na watu wa hali mbalimbali wa Mali.

Bw. Sautu Badian Kouyate mwenye umri wa miaka 80 ni mmojawapo wa waanzilishiji wa nchi ya Mali ambaye pia alisaini makubaliano ya ushirikiano wa matibabu kati ya China na Mali. Alipokumbusha misaada ya matibabu iliyotolewa na China kwa Mali katika miaka 40 iliyopita, alisema imepata mafanikio halisi. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa: "kikundi cha madaktari cha China kilituletea matibabu ya zama za hivi leo na matibabu ya kijadi ya China, madaktari wa China ni wazuri, walitibu wagonjwa wengi na pia waliwafanya wananchi wa Mali waijue China vizuri zaidi."

Naibu mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa katika wizara ya mambo ya nje ya Mali Bw. Mamunu Toure aliwahi kutibiwa na madaktari wa China na aliona matibabu ya madaktari wa China ni ya kiwango cha juu. Alisema madaktari wa China kila siku wanafanya juhudi kuwatibu wagonjwa na wana sifa nzuri nchini Mali.

"madaktari wa China ni muhimu sana kwa sisi!" alisema, "China inatusaidia sana katika sekta ya matibabu, hivyo kiwango cha matibabu cha Mali kimeinuka sana."

Waziri wa afya wa Mali Bw. Oumar Ibrahima Toure alipokutana na ujumbe wa wizara ya afya ya China pia alisifu sana misaada ya matibabu ya China na alisema madaktari wa China walitoa huduma nzuri za matibabu kwa wananchi wa Mali na kupendwa na wananchi wa Mali. Akisifu alisema: "madaktari wa China waliwasaidia madaktari wa Mali na kutoa tekenolojia na ujuzi wao, hii ndiyo sababu ambayo tunasherehekea kwa furaha miaka 40 tangu China itoe msaada wa matibabu kwa Mali."

Waziri huyo pia alisema, Mali inajenga hospitali mpya na kuzingatia kukusanya madaktari wa China nchini Mali ili kuwahudumia wananchi wa Mali.

Siku moja katika mwaka 2008, dakari mmoja wa China aliumwa huko Markala nchini Mali. Siku iliyofuata, watu wengi wa sehemu hiyo waliopata habari hiyo na walikwenda kumpa pole. Daktari huyo anaitwa Hong Jianfei ambaye ni daktari mmoja wa kikundi cha madaktari wa China huko Markala na pia ni daktari wa kwanza wa kitengo cha mifupa wa China kwenye hospitali ya Markala.

Wakazi wa huko wana tabia ya kulala kwenye mkeka, kwa hivyo wazee wengi wanaumwa na kiuno au miguu. Kwa kutumia vyombo vya kisasa vilivyopo kwenye kitengo cha mifupa, daktari Hong ametibu wagonjwa wengi, na alijulikana sana siku hadi siku, wagonjwa wa nchi jirani walikuja kutibiwa na daktari Hong kutoka sehemu za mbali, sasa hospitali ya Malkala imakuwa kiini cha kitengo cha magonjwa ya mifupa.

Mwandishi wa habari wa China aliambatana na ujumbe wa wizara ya afya ya China kutembelea hospitali hiyo na kukutana na Bw. Hong Jianfei, ambapo alikuwa akipima tena mgonjwa mwanamke aliyefanyiwa upasuaji siku moja kabla ya hapo. Mgonjwa huo alisema upasuaji ulifanywa na daktari Hong kwa ustadi mkubwa.

Wasaidizi wanawake wa Bw. Hong Jianfei pia walisema, kiwango cha matibabu ya daktari Hong ni cha juu, yeye anafanya kazi bila ya kupumzika, wakazi wa huko walitiwa moyo wake wa kufanya kazi kwa bidii. Walisema, daktari Hong ni mtu maarufu huko Malkala, wazee wa huko wanampenda sana. Muda wa daktari Hong utamalizika baada ya miezi 10, lakini watu wa huko wanataka yeye aendelee kukaa kwa sababu ameokoa watu wengi.

Daktari Hong Jianfei alipohojiwa kwa nini alifanya kazi kwa bidii bila kusita, alijibu kwa fahari: " ninaona furaha kutoa mchango kwa wananchi wa Mali. Tulipowatibu wagonjwa wengi, wakazi wa huko hutusifu na kusema: wachina ni wazuri sana!"

Mgonjwa mmoja anayeitwa Saydu Fane alisema, daktari wa China alimpa maisha kwa mara ya pili. Alisema watu wengi walikuja kutibiwa kwa sababu kuna madaktari wa China kwenye hospitali ya Markala, na ustadi wa madaktari hao ni wa kiwango cha juu na wanatoa dawa bure na kuonesha moyo wa kuwaokoa na kuwatibu watu.

Kaimu wa mkuu wa hospitali hiyo Bibi Kulibali pia alitiwa moyo sana na urafiki wa dhati wa madaktari wa China kwa wananchi wa Malkala. Alisema: " Madaktari wa China walifanya kazi nyingi za hospitali ya Malkala, kama hakuna madaktari hao kutoka China, hospitali hiyo haitakuwepo. Madaktari wa China wanapokea wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali za Mali na wajulikana sana nchini Mali. Wao ni madaktari wazuri wa wananchi wa Mali."

Kabla ya miaka 40 iliyopia, kikundi cha kwanza cha madaktari wa China waliosaidia Mali kilifanya kazi kwenye hospitali ya Malkala. Hivi sasa, kikundi cha 20 cha madaktari wa China kinachosaidia Mali kilifanya kazi kwenye hospitali za Kadi, Sikaso na Malkala. Kuna wanachama 31, licha ya wakalimani watatu, wengine walitoka mkoa wa Zhejiang.

Mali ni moja ya nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo duniani, malaria, kipindupindu, homa na ugonjwa wa ukimwi ni maradhi ambapo yameenea sana, madaktari wa China walitatua matatizo ya upungufu wa vifaa vya matibabu na madawa na kusifiwa sana na watu wa huko kwa ustadi wa kiwango cha juu na moyo wa kutoa mchango bila ya kujali maslahi yao wenyewe.