Mkutano wa wakuu wa nchi wa kundi la nchi 20 kuhusu soko la fedha na uchumi wa dunia ulifanyika tarehe 15 huko Washington, mji mkuu wa Marekani. Rais Hu Jintao wa China alihudhuria mkutano na kutoa hotuba isemayo "Tuondoe matatizo kwa kuimarisha ushirikiano, ambayo ilifafanua chanzo cha msukosuko wa fedha, na kueleza msimamo wa China kuhusu baadhi ya masuala nyeti ya duniani yakiwemo namna ya kuukabili msukosuko wa fedha na kufanya mageuzi juu ya utaratibu wa mambo ya fedha wa dunia.
Msukosuko wa fedha uliosababishwa na msukosuko wa utoaji mikopo ya ngazi ya pili uliotokea Marekani, unaenea duniani. Msukosuko huo mkubwa umeenea kwenye maeneo makubwa, kuleta athari kubwa na kwa nguvu, ambao haujaonekana tokea miaka ya 30 ya karne iliyopita. Nchi zote duniani zinapaswa kutafakari chanzo cha kutokea msukosuko huo wa fedha. Bw. Hu Jintao alisema, jambo la haraka la kufanywa na jumuiya ya kimataifa ni kuendelea kuchukua hatua zote za mwafaka, kurejesha imani ya watu kuhusu masoko na kuzuia kuenea kwa msukosuko wa fedha. Nchi muhimu za viwanda zinapaswa kubeba majukumu na wajibu wao, kutekelza sera za mwafaka, kutuliza masoko yake ya fedha na ya kimataifa na kulinda maslahi ya wawekezaji. Kwa upande mwingine, nchi mbalimbali zinatakiwa kuimarisha uratibu wa sera za uchumi wa taifa, kuimarisha upashanaji habari kuhusu mambo ya uchumi na fedha, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu usimamizi wa mambo ya fedha, na kuanzisha mazingira ya kutuliza masoko ya fedha ya kila nchi na ya kimataifa.
Bw. Hu Jintao alisisitiza, kudumisha ongezeko la uchumi ni msingi wa kuukabili msukosuko wa fedha. Nchi mbalimbali zinatakiwa kurekebisha sera za uchumi za taifa ili kuhimiza ongezeko la uchumi na kuepusha uzorotaji wa uchumi wa dunia. Aidha, pande mbalimbali zinatakiwa kuchukua hatua kwa pamoja ili kutuliza masoko ya nishati na nafaka ya dunia, kuzuia ulanguzi na kuanzisha mazingira bora kwa maendeleo ya uchumi. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuzuia uwekaji wa vizuizi vya biashara na uwekezaji, na kujitahidi kufanikisha mazungumzo ya biashara ya duru la Doha.
Kuhusu mageuzi ya utaratibu wa mambo ya fedha ya dunia yanayofuatiliwa na pande mbalimbali, Bw. Hu Jintao alisisitiza kuwa usawa, haki, kuvumiliana na utaratibu mzuri ni mwelekeo mpya wa maendeleo ya utaratibu wa fedha wa dunia. Alisema, mageuzi ya utaratibu wa mambo ya fedha wa dunia yanatakiwa kufanywa kwa kufuata kanuni nne ambazo zitatekelezwa kwa pande zote, uwiano, hatua kwa hatua na yenye ufanisi. Kuhusu hayo, Bw. Hu Jintao alipendekeza hatua nne za mageuzi:
Kwanza, kuimarisha ushirikiano kuhusu usimamizi wa kimatiafa juu ya mambo ya fedha ya dunia; Pili, kuendeleza mageuzi juu ya mashirika ya fedha ya dunia; Tatu, kuhimiza ushirikiano wa mambo ya fedha wa kikanda; Na nne, kuhimiza kwa hatua imara kuweko mifumo mingi ya fedha ya kimatiafa.
Rais Hu Jintao alisisitiza, katika mazingira, ambayo utandawazi wa uchumi unaendelezwa kwa kina kirefu, uhusiano wa mambo ya fedha wa nchi mbalimbali unaimarishwa siku hadi siku. Msukosuko huo wa fedha si unaathari vibaya masoko ya fedha ya nchi zilizoendelea, bali pia unaathiri kwa viwango tofauti nchi zinazoendelea. Alisema, jumuiya ya kimataifa, hususan nchi zilizoendelea zinatakiwa kuchukua hatua halisi za kuzisaidia nchi zinazoendelea, hasa nchi za Afrika kuondokana na matatizo. Mashirika ya fedha, nayo yanatakiwa kutoa misaada kwa haraka kwa nchi zilizoendelea, ambazo zimeathiriwa vibaya na msukosuko wa fedha. Alisema, nchi zilizoendelea zinatakiwa kuendelea kutekeleza ahadi zilizotoa, kusamehe madeni ya nchi zilizoko nyuma kimaendeleo.
Bw. Hu Jintao pia aliwafahamisha viongozi washiriki maendeleo ya uchumi wa China, alisema, China inapenda kushiri kuhifadhi utulivu wa mambo ya fedha ya dunia, na kutoa uungaji mkono mkubwa zaidi kwa nchi zinazoendelea, ambazo zimeathirika katika msukosuko wa fedha, na kushiriki mpango wa ukusanyaji fedha za biashara wa Benki ya Dunia na mashirika ya ukusanyaji fedha ya kimataifa.
|