Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-17 18:58:03    
China kuunganisha ujenzi wa mazingira ya kiikolojia kwenye shughuli za kupanua matumizi ya bidhaa nchini

cri

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang hivi karibuni alisema, ili kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, China itaunganisha kazi za kuboresha maisha ya watu na ujenzi wa mazingira ya kiikolojia, na kuchukua kazi za kupunguza utoaji wa uchafuzi na kubana matumizi ya nishati kuwa sehemu muhimu katika shughuli za kupanua matumizi ya bidhaa nchini.

Bw. Li Keqiang alisema, katika miaka 30 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera za mageuzi na kufungua mlango kwa nje, pamoja na kudumisha ongezeko la kasi la uchumi, China pia imepunguza kiasi hali ya uchafuzi wa mazingira, na mazingira ya baadhi ya sehemu na miji yameboreka. China imefanya juhudi kubwa kwa katika shughuli za kuhifadhi mazingira.