Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-17 19:49:46    
Mafanikio aliyoyapata spika Wu Bangguo katika ziara ya barani Afrika

cri

Baada ya kumalizika kwa ziara ya spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo, katika nchi 5 za Afrika, naibu spika Bw. Cao Weizhou, ambaye aliandamana naye katika ziara hiyo, alisema, ziara hiyo ya Bw. Wu Bangguo imeimarisha mawasiliano ya viongozi wa China na wa nchi za Afrika, kuhimiza utekelezaji wa hatua za matokeo ya mkutano wa Beijing wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika , na kuongeza mambo mapya ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa China na Afrika.

Kutokana na mwaliko, spika wa bunge la umma la China, Bw. Wu Bangguo alifanya ziara ya kirafiki katika nchi za Algeria, Gabon, Ethiopia, Madacasca na Shelisheli kuanzia tarehe 3 hadi 15 mwezi Novemba, katika ziara hiyo alitembelea pia kamati ya Umoja wa Afrika iliyoko Adisababa, mji mkuu wa Ethiopia, na kushiriki sherehe ya uanzishaji wa ujenzi wa kituo cha mikutano cha Umoja wa Afrika, ambacho kinajengwa kwa msaada wa China.

Kuhusu ziara hiyo ya Bw. Wu Bangguo katika nchi 5 za Afrika, naibu spika Bw. Cao Weizhuo alisema, uhusiano kati ya China na nchi hizo 5 ni kama mfano wa uhusiano wa China na Afrika, unaonesha kuwa uhusiano wa China na Afrika ni wa pande mbalimbali, muda mrefu na wa aina nyingi. Katika ziara hiyo, Bw. Wu Bangguo alifanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na marais, spika, na mawaziri wakuu wa nchi hizo 5 pamoja na mwenye kiti wa kamati ya Umoja wa Afrika, ambapo walibadilishana maoni na kufikia kwenye mwafaka kuhusu kuimarisha hali ya kuaminiana, ushirikiano wa kunufaishana, kuinua kiwango cha kusaidiana na maingiliano ya mabunge ya nchi hizo kwa lengo la kimkakati la kukuza maendeleo ya uhusiano wa China na Afrika, alisema, ziara hiyo imepata mafanikio muhimu.

Katika upande wa kuimarisha hali ya kuaminiana, katika kila nchi aliyofika Bw. Wu Bangguo, alipongeza uhusiano wa urafiki na ushirikiano wa nchi mbili, alisema, hata mambo ya dunia yabadilike namna gani, China na Afrika zitatendeana kwa usawa, kuaminiana, kuelewana na kuungana mkono katika masuala nyeti yanayofuatiliwa na upande mwingine. Viongozi wa nchi 5 walisisitiza kushikilia sera za kuweko kwa China moja tu duniani, kupongeza na kuunga mkono umuhimu wa China katika mambo ya kimataifa. Walisema, China ni rafiki wa kutegemeka na mwenzi wa kidhati katika ushirikiano, ziara ya Bw. Wu Bangguo itaimarisha nia na imani za nchi za Afrika za kufanya ushirikiano wa kunufaishana na China katika maeneo mengi zaidi.

Katika upande wa kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, Bw. Wu Bangguo anafuatilia sana ushirikiano wa uchumi na biashara wa China na Afrika, alipokuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi alizozitembelea, alitumia wakati mwingi kujadili uimarishaji wa maeneo na miradi muhimu ya ushirikiano wa uchumi na biashara wa pande mbili. Kuhusu hali ya hivi sasa ya ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika, Bw. Wu alipendekeza kukuza umuhimu wa kampuni na viwanda, mambo ambayo ni muhimu zaidi katika ushirikiano wa uchumi na biashara, na kujitahidi kupata maendeleo mapya katika baadhi ya miradi mikubwa ya ushirikiano yakiwemo uendelezaji wa matumizi ya rasilimali za nishati, ujenzi wa miundo-mbinu na ujenzi wa kanda ya ushirikiano wa uchumi na biashara ili kufanya miradi hiyo mikubwa kuwa mambo muhimu na ukuaji wa ushirikiano wa uchumi na biashara wa China na Afrika. Viongozi wa nchi 5 za Afrika walisema, watahimiza utekelezaji wa miradi mikubwa iliyofikia mapatano kati ya pande mbili na kukaribisha viwanda vingi zaidi vya China viende huko kushiriki uendelezaji wa matumizi ya rasilimali za nishati na ujenzi wa miundo-mbinu.

Katika upande wa kuinua kiwango cha kusaidiana, Bw. Wu alisema, China itaendelea kuongeza misaada kwa nchi za Afrika na kuwanufaisha kihalisi watu wake. Alisema, China itazidisha uagizaji bidhaa kutoka Afrika, na kuzidisha uwekezaji katika bara hilo.

Mwishoni, naibu spika Bw. Cao alisema, vyombo vya habari vya nchi 5 za Afrika vilitoa habari nyingi kuhusu ziara ya spika wa bunge la umma la China, mambo ambayo yanachangia uimarishaji wa uhusiano mpya wa kiwenzi na kimkakati wa China na Afrika.