Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-17 19:53:47    
Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 waongeza imani za nchi za kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani

cri

Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 kuhusu soko la fedha na uchumi wa dunia ulifungwa jumamosi iliyopita nchini Marekani. Watalaamu wa China wamesema, ingawa mkutano huo haukutoa mpango mzuri wa kukabiliana na msukosuko wa fedha, lakini taarifa iliyotolewa na pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo imeongeza imani za nchi mbalimbali za kukabiliana na msukosuko.

Kwenye mkutano huo, viongozi wa nchi muhimu zilizoendelea na nchi zinazoendelea waliamua kwa kauli moja kuwa ni lazima kuchukua vitendo vya kisera kuhusu mambo mengi kwenye msingi wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, ili kupunguza athari ya msukosuko wa fedha na athari ya kupungua kwa ongezeko la uchumi duniani, tena kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea. Mkutano huo pia umezitaka nchi mbalimbali duniani zitekeleze sera za lazima kuhusu mambo ya fedha na sarafu ili kudumisha ongezeko la uchumi, ambapo washiriki wa mkutano huo walifikia kanuni tano kuhusu mageuzi ya mfumo wa fedha wa Kimataifa, lakini hatua halisi zitakamilishwa zaidi kabla ya mwishoni mwa mwezi Machi mwakani.

Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti wa mambo ya uchumi wa China katika Chuo kikuu cha Fudan cha Shangha Bw. Zhang Jun alisema, mchango mkubwa wa mkutano huo ni kuimarisha imani. Alisema:

Mkutano huo umeimarisha imani za kwenye nchi mbalimbali duniani katika kufanya ushirikiano na kuchukua hatua za kuzuia zaidi msukosuko wa fedha usienee, hasa kuzuia hali ya kudidimia kwa uchumi katika makundi ya uchumi.

Hivi sasa nchi zilizoendelea zimechukua sera za kupunguza faida ya akiba benkini na kupunguza riba ya mikopo benkini ili kusaidia ongezeko la uchumi, na mkutano huo umedhihirisha wazi kuwa nchi mbalimbali duniani zinapaswa kutekeleza sera za lazima kuhusu mambo ya fedha ili kuhimiza juhudi za kuendeleza mambo ya uchumi. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, China ilitangaza mpango wake wa kutenga yuan trilioni 4 kwa ajili ya kuhimiza juhudi za kuendeleza mambo ya uchumi, mpango huo umehimiza pia juhudi za nchi nyingine duniani.

Bw. Zhang Jun alisema, hatua ya China ina umuhimu wake wa kuigwa na nchi nyingine duniani. Alisema: 

Mpango huo wa China umezungumzwa na watu wengi hata kwenye mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20, mpango huo umezipa ishara ya kuigwa nchi nyingi zinazoendelea, na pia utaleta athari nzuri kwa uchumi wa dunia nzima.

Aidha, viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo walifikia maoni ya pamoja kuhusu kanuni kadha wa kadha juu ya mageuzi ya mfumo wa fedha wa Kimataifa. Kwa kufuata kanuni hizo, miundo ya mambo ya fedha ya Kimataifa itaundwa upya, na itawapokea nchi wanachama wengi wa makundi ya uchumi yaliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni, kama vile China, Brazil na India, nchi hizo zitaonesha umuhimu wao mkubwa zaidi katika mfumo wa fedha wa Kimataifa; wakati huo huo utaratibu wa usimamizi wa mambo ya fedha na kanuni za uhasibu kwenye eneo la dunia zitafanyiwa mageuzi, na kundi la nchi 20 litaanzisha Umoja wa usimamizi ili kusimamia mashirika makubwa ya fedha kote duniani.

Kwenye mkutano huo, China imetarajiwa kuonesha umuhimu wake mkubwa zaidi katika mageuzi ya mfumo wa fedha wa Kimataifa. Rais Hu Jintao wa China amesema wazi kwenye mkutano huo kuwa, China inapenda kuendelea kufuata msimamo wa kuwajibika na kujiunga na ushirikiano wa Kimataifa unaolenga kulinda utulivu wa mambo ya fedha duniani na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia.

Mtaalamu mkuu wa elimu ya uchumi wa J.P.Morgan Chase kwenye kanda ya Asia na Pasifiki Bw. Gong Fangxiong alisema, katika wakati huu wa sasa China inatakiwa kufanya juhudi zaidi za kutoa mchango kwa ajili ya ufufuzi wa uchumi wa dunia nzima, pia China inapaswa kujipatia haki ya kutoa maoni na mapendekezo inayolingana na mchango wake.

Alisema: 

China ingeshiriki kwa hiari kwenye juhudi za Kimataifa, huku ikijitahidi kujipatia hadhi na haki tunayostahiki kupata. Tukitoa pesa, pesa hizo zitatumika namna gani, kama huna haki ya kutoa maoni na mapendekezo hutaweza kuwa na nguvu ya ushawishi.