Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao hivi karibuni amefanya ukaguzi kwenye sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Sichuan, ambapo amekwenda nyumbani kwa wakulima, viwanda na shule kuwatembeela watu na kukagua hali ya ukarabati wa sehemu baada ya maafa.
Hii ni mara ya 6 kwa waziri mkuu huyo kwenda sehemu zilizokumbwa na maafa. Naye amesisitiza kuwa, kuharakisha kazi ya ufufuzi na ukarabati wa sehemu baada ya maafa ni hatua kubwa katika kazi za hivi sasa za kupanua mahitaji ya soko nchini na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi, pia ni kazi kuu ya sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi.
Bw. Wen Jiabao amefuatilia sana suala la kupita salama siku za baridi kwa wakazi wa sehemu zilizokubmwa na maafa, na amesisitiza kuharakisha kazi ya kujenga nyumba za kudumu kwa kufuata kanuni zilizowekwa.
|