Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-18 09:57:47    
Rais Hu Jintao awasili Havana na kuanza ziara yake nchini Cuba

cri

 

Rais Hu Jintao wa China amewasili Havana, mji mkuu wa Cuba tarehe 17 usiku kwa saa za huko, na kuanza ziara yake nchini Cuba.

Kwenye uwanja wa ndege rais Hu alitoa hotuba ya maandishi akisema anafurahi kufanya ziara kwa mara nyingine nchini Cuba.

Rais Hu alisema wananchi wa China na Cuba wamekuwa na urafiki mkubwa miaka mingi iliyopita, kuimarisha na kuendeleza urafiki kati ya China na Cuba ni matakwa ya pamoja ya wananchi wa nchi hizo mbili. Alisema lengo la ziara yake ni kuongeza urafiki, kupanua ushirikiano, na kujenga mustakabali mzuri wa ushirikiano pamoja na ndugu wa Cuba.

Siku hiyo alasiri, rais Hu alimaliza ziara yake nchini Costa Rica. Katika ziara hiyo, rais Hu amekutana na rais Oscar Arias Sanchez wa Costa Rica na mwenyekiti wa baraza la kutunga sheria la nchi hiyo Bw. Francisco Antonio Pacheco. Pande hizo mbili zimesaini nyaraka nyingi za ushirikiano na kufikia makubaliano kuhusu kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.