Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-18 19:06:27    
Ziara ya rais Hu Jintao wa China katika nchi za Latin Amerika itasukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili

cri

Rais Hu Jintao wa China alifanya ziara nchini Costa Rica kuanzia tarehe 16 hadi 17 mwezi huu. Baadaye rais Hu atatembelea Cuba na Peru, na pia atahudhuria mkutano wa 16 usio rasmi wa wakuu wa Shirika la ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasikifiki utakaofanyika nchini Peru.

China na Costa Rica zilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi tarehe 1 Juni mwaka 2007, tangu hapo uhusiano kati ya pande hizo mbili unaendelezwa kwa kasi. Mwezi Oktoba mwaka jana rais Oscar Arias Sanchez wa Costa Rica alifanya ziara nchini China na kupata mafanikio. Na safari hii ni mara ya kwanza kwa rais Hu Jintao wa China kufanya ziara nchini Costa Rica. Mtafiti wa Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Xu Shicheng alisema:

Ziara hiyo ya rais Hu itasukuma mbele uhusiano kati ya China na Costa Rica na kati ya China na Latin Amerika, ambapo nchi hizo mbili zitasaini makubaliano 11, na marais wa nchi hizo mbili watatangaza kuwa nchi hizo mbili zitaanzisha mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huria. Ziara hiyo ya rais Hu itahimiza zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na Costa Rica.

Bw. Xu alisema, katika sehemu ya Amerika ya kati bado kuna nchi kadhaa ambazo hazijaanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Serikali ya China tarehe 5 mwezi huu ilitoa "Waraka wa sera za China juu ya Latin Amerika na Cariebbean", na ziara ya safari hii ya rais Hu Jintao wa China nchini Costa Rica, yote hayo yametoa ishara kwa nchi zilizoko sehemu hiyo kuwa, China inapenda kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa kibalozi na nchi mbalimbali za Latin Amerika hasa nchi za Amerika ya kati.

Bw. Xu alisema:

Kama "Waraka wa sera za China juu ya Latin Amerika na Cariebbean" ulivyosema, China inapenda kuendeleza uhusiano wa kibalozi na nchi za Amerika ya kati kwenye msingi wa kuwepo kwa China moja. Na hatupingi Taiwan kufanya biashara na nchi za Amerika ya kati. Nina imani kuwa, ziara ya rais Hu nchini Costa Rica itahimiza pia maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi nyingine za Amerika ya kati.

Mkurugenzi wa kitivo cha uhusiano wa Kimataifa katika chuo kikuu cha Catholic cha Salta cha Algentina Bw. Martin A. Rodiguez ambaye amefanya utafiti kuhusu uhusiano kati ya China na Latin Amerika kwa miaka mingi alisema, nguvu ya ushawishi ya China katika Bara la Latin Amerika ina umuhimu mkubwa kwa ajili ya kuhimiza mambo ya uchumi na biashara ya sehemu ya Asia na Pasifiki yaendelezwe kwa utaratibu katika hali ya masikilizano. Alisema:

Naona ziara hiyo ya rais Hu Jintao wa China katika nchi za Latin Amerika ni ya kufaa sana, ameleta imani na matumaini kwa nchi za Latin Amerika juu ya maendeleo ya miaka kadhaa ijayo. Ziara yake na "Waraka wa sera za China juu ya Latin Amerika na Cariebbean" uliotolewa na serikali ya China hata zimezifanya bei za mazao ya kilimo yanayouzwa na nchi za Latin Amerika kupanda upya kwenye soko la Kimataifa, na kuondoa wasiwasi wa nchi za Latin Amerika. Hii imeonesha kuwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya sisi wa nchi za Latin Amerika na China utaendelea kukuzwa kwa utulivu.

Bw. Rodriguez alisema, katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano kati ya China na nchi za Latin Amerika unaendelezwa kwa hatua madhubuti, nchi nyingi zaidi za Latin Amerika zinataka kuvutia vitega uchumi vya kamapuni za China. Amedhihrisha kuwa, China imeleta fursa ya kujiendeleza kwa nchi za Latin Amerika. Alisema, uchumi wa China unaendelezwa siku hadi siku, mahitaji ya soko la China ya kuagiza bidhaa kutoka nchi za nje yanaongezeka siku hadi siku, hivyo bidhaa nyingi za Latin Amerika zinaweza kukidhi mahitaji hayo ya soko la China. Katika hali ya kukabiliwa na msukosuko wa fedha kwa hivi sasa, China inashikilia kuzifungulia mlango nchi za nje, hii ni fursa nzuri ya kujiendeleza kwa nchi za Latin Amerika. Alisema, ziara ya rais Hu imeonesha imani na dhamira ya China ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi za Latin Amerika, na nchi za Latin Amerika zinapaswa kushika fursa na kuanzisha ushirikiano na China.