Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-18 20:28:47    
China kuchukua hatua zenye nguvu zaidi ili kuhakikisha usalama wakati wa uzalishaji

cri
Naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Dejiang tarehe 18 hapa Beijing amesema, serikali ya China itachukua hatua zenye nguvu zaidi za kuhakikisha usalama wakati wa uzalishaji.

Bw. Zhang amesema serikali ya China itaimarisha ujenzi wa sheria na utaratibu kuhusu usalama wakati wa uzalishaji, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa usalama wakati wa uzalishaji, kutenga fedha zaidi katika eneo hili, kueneza vifaa vyenye usalama, kuanzisha kampeni ya ujenzi wa kwa kufuata vigezo vya usalama, kuongeza nguvu za kushughulikia gesi kwenye migodi ya makaa ya mawe, na kurekebisha na kufunga migodi midogo ya uchimbaji wa makaa ya mawe.

Bw. Zhang amesema hali ya usalama wakati wa uzalishaji imeboreshwa nchini China katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado inakabiliwa na changamoto kubwa.