Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-19 14:27:07    
Rais Hu Jintao amtembelea katibu wa kwanza wa kamati ya chama cha kikomunisti cha Cuba Bw. Fedel Castro

cri

Rais Hu Jintao wa China tarehe 18 huko Havana alimtembela katibu wa kwanza wa kamati ya chama cha kikomunisti cha Cuba Bw. Fedel Castro, viongozi hao wawili walizungumza kwa muda mrefu.

Rais Hu alipeleka salamu za chama cha kikomunisti cha China kwa Bw. Castro, na kusema viongozi wa kizazi baada ya kizazi wa China na Bw. Castro walianzisha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Cuba ambao umefanikiwa kupita mabadiliko ya siasa duniani, urafiki kati ya nchi hizo mbili na vyama hivi viwili umetia mizizi mioyoni mwa wananchi wa nchi hizo mbili.

Bw. Castro alimkaribisha kwa furaha rais Hu Jintao kutembelea tena nchini Cuba. Alisema msukosuko wa fedha unaenea siku hadi siku duniani, lakini uchumi wa China bado unaendelezwa vizuri, hii inaonesha China ni nchi inayofanya matayarisho mazuri zaidi. Chama, serikali na wananchi wa Cuba wataendelea kuungana na chama, serikali na wananchi wa China katika kusukuma mbele mambo ya kirafiki kati ya nchi hizo mbili.