Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-19 17:33:44    
Bw. He Guoqiang awataka wafanyabiashara wa nje waimarishe imani yao ya kuwekeza nchini China

cri

Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisiti cha China Bw. He Guoqiang alifanya ukaguzi mkoani Guangdong kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 18 mwezi huu. Alipotembelea tawi la kampuni ya ya China ya Dupont huko Shenzhen Bw. He Guoqiang aliwatia moyo wafanyabiashara wa nje waimarishe imani yao ya kuwekeza nchini China, pia aliwataka maofisa wa miji na wa mkoa huo waitishe kongamano na makampuni ya nje ili kusikiliza maoni na mapendekezo yap.

Kuhusu kukabiliana na athari mbaya ya msukosuko wa fedha duniani, Bw. He Guoqiang alizitaka kamati za chama na serikali katika ngazi mbalimbali zitekeleze kithabiti sera na mpango uliowekwa na serikali kuu ya China, kuongeza uwekezaji na kuboresha muundo wa uwekezaji, pia idara hizo zinatakiwa kuweka mkazo katika kupanua mahitaji ya matumizi, kuharakisha marekebisho ya muundo wa uchumi na kubadilisha njia ya maendeleo, kuendelea kuimarisha mageuzi na kufungua mlango zaidi kwa nje, na kuhakikisha na kuboresha kihalisi maisha ya watu.