Gazeti la Renminribao la China tarehe 19 mwezi huu limechapisha hotuba aliyotoa waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao tarehe 7 mwezi huu kwenye kongamano la ngazi ya juu kuhusu kuendleeza na kuhamisha teknolojia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, Bw. Wen Jiabao alisema, hivi sasa hali ya msukosuko wa fedha imeenea zaidi kote duniani, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha zaidi ushirikiano ili kukabiliana kithabiti na mabdiliko ya hali ya hewa.
Bw. Wen Jiabao alisema, hivi sasa China iko kwenye kipindi cha maendeleo ya kasi ya utandawazi wa viwanda,wastani wa utoaji hewa inayosababisha kuongezeka kwa halijoto wa kila mtu nchini China haufikii theluthi moja ya ule wa nchi zilizoendelea. Hivi sasa China inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka pande za kuendeleza uchumi, kuondoa umaskini na kupunguza kasi ya utoaji hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani. Serikali ya China itafuata kithabiti njia za uzalishaji, maisha na matumizi zinazosaidia kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira, ili kusukuma mbele jamii nzima ifuate njia ya maendeleo endelevu yenye hali nzuri ya uzalishaji, maisha bora na mazingira mazuri ya kiikolojia.
|