Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-20 18:01:19    
Mazungumzo kuhusu suala la Georgia yapata maendeleo

cri

Mkutano wa pili kuhusu suala la Georgia, ambao uliandaliwa na Umoja wa Mataifa, jumuiya ya usalama ya Ulaya na Umoja wa Ulaya ulifanyika tarehe 19 katika Jumba la Palais Des Nations kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Ulaya mjini Geneva. Wawakilishi kutoka nchi za Russia na Georgia walikuwa na mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mapigano kati ya pande mbili mwezi Agosti mwaka huu, wakati mikutano ya vikundi viwili vya kazi kuhusu masuala ya wakimbizi na usalama ilipata baadhi ya maendeleo.

Mkutano huo wa siku moja ulikuwa wa faragha. Saa 9 ya alasiri ya siku hiyo, balozi maalumu wa Umoja wa Ulaya kuhusu suala la Georgia Bw. Pierre Morel aliwaanbua waandishi wa habari kuwa, siku hiyo haukufanyika mkutano wa wajumbe wote, isipokuwa ilifanyika mikutano miwli ya vikundi viwili vya kazi, kwa nyakati tofauti ilijadili suala la kuwarejesha na kuwapanga wakimbizi waliokimbia makwao katika mapigano, na suala la kudumisha usalama na utulivu kwenye sehemu ya Caucasus. Vilevile alisoma taarifa ya mkutano kuhusu mambo maneno, na kupongeza sana mafanikio ya mikutano. Taarifa ilisema, mikutano ilithibitisha utaratibu wa kuunda vikundi viwili vya kazi, ukiwa kanuni ya kutatua suala la Georgia katika siku za baadaye, na kuamua kufanya mkutano wa 3 mjini Geneva, tarehe 17 na 18 mwezi Desemba.

Siku hiyo, wajumbe wa nchi 8 walishiriki mikutano ya vikundi viwili. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na jumuiya ya usalama ya Ulaya zikiwa wasuluhishi, Russia, Georgia na Marekani, pamoja na wawakilishi wa Ossetia ya kusini na Abkhazia walihudhuria kwenye mkutano huo. Kiongozi wa ujumbe wa Russia ni naibu waziri wa mambo ya nje Bw. Grigory Karasin, na kiongozi wa ujumbe wa Marekani ni Bw. Daniel Fried ambaye ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Tarehe 15 mwezi Oktoba, pande mbalimbali zilikuwa na mkutano wa kwanza kuhusu suala la Georgia katika Jumba la Palais Des Nations, lakini ulifungwa bila mafanikio yoyote, kutokana na kuwa Russia ilishikilia kutaka mkutano huo kuwaruhusu wawakilishi wa Ossetia ya kusini na Abkhazia wahudhurie mkutano wa wajumbe wote, hatimaye iliondoka mkutanoni kutokana na kutotimizwa kwa sharti hilo. Upande ulioandaa mkutano huo, ulitumia sana akili ya kidiplomasia, haukuitisha mkutano wa wajumbe wote ili kuepusha kushindwa kwa mkutano huo, bali uliitisha mikutano ya vikundi vya kazi ili kukwepa suala nyeti la hadhi ya Ossetia ya kusini na Abkhazia, na kufanya pande mbalimbali zishiriki mazungumzo. Pande mbalimbali zilitoa pongezi kwa hatua hiyo iliyochukuliwa. Habari zilisema, washiriki wa mkutano walifikia kwenye mwafaka kuhusu mambo mawili. La kwanza, zijitahidi kutoa misaada kwa wakimbizi elfu 30, kutoa misaada ya kuwarejesha makwao na kutoa vitu vya msaada vikiwemo mahema kabla ya siku za baridi kufika; Pili ni kuheshimu usimamishaji wa vita uliotimizwa hivi sasa na kuhakikisha usalama wa pande mbalimbali.

Pande mbalimbali zimetambua kuwa hali ya usalama kwenye sehemu ya Caucasus si ya kuridhisha. Russia inasisitiza, Georgia isizishambulie tena Ossetia ya kusini na Abkhazia hapo baadaye, na kutaka jumuiya ya kimataifa kutoipa Georgia silaha. Vyombo vya habari vinasema, mkutano huo ni mwanzo mzuri kwa utatuzi wa suala la Georgia, makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano yanasaidia pande mbalimblai kufanya ushirikiano na kuanzisha hali ya kuaminiana. Yapaswa kuona vilevile kuwa masuala likiwemo la utoaji misaada ya ubinadamu, ni rahisi kufikia kwenye mwafaka, lakini suala la usalama la sehemu ya Caucasus ni suala gumu lenye mgongano mkubwa, hivyo utatuzi wa suala la Georgia utakuwa ni kazi kubwa ya muda mrefu.