Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-20 19:22:21    
Masuala ya usalama wa chakula na sifa za bidhaa yatakiwa kutatuliwa kwa mazungumzo kati ya China na Marekani

cri
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Qin Gang amesema, China inapenda masuala kuhusu usalama wa chakula na sifa za bidhaa yatatuliwe kwa kupitia mazungumzo yenye usawa kati ya China na Marekani.

Hivi karibuni Marekani ilitangaza marekebisho ya sheria ya usalama wa bidhaa, ambayo yanataka upande wa tatu kufanya upimaji wa bidhaa. Kuhusu tukio hilo, Bw. Qin Gang amesema, China imeanzisha mfumo kamili wa upimaji wa bidhaa zinazosafirisha nje, bidhaa zinazoorodheshwa kwenye orodha ya ukaguzi na karantini ni lazima zifanyiwe upimaji kabla ya kusafirishwa nje, na bidhaa zinazoshindwa kupita upimaji huo haziruhusiwi kuuzwa nje ya China.

Msemaji huyo ameongeza kuwa, idara za ukaguzi za sifa za bidhaa za China na maabara nyingi zinafanya upimaji huria, nazo zina zana za kisasa na kufuata mfumo wa kisasa wa usimamizi, kwa hiyo zinaweza kufanya ukaguzi kwa haki na huria na zina sifa zinazolingana na masharti ya Marekani kuhusu taasisi za kufanya upimaji za upande wa tatu.