Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-21 18:16:58    
Ukarabati waendelea vizuri katika mkoa wa Sichuan uliokumbwa na tetemeko la ardhi

cri

Naibu mkuu wa mkoa wa Sichuan Bw. Wei Hong tarehe 21 hapa Beijing amesema, ukarabati unaendelea vizuri katika sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Sichuan.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na ofisi ya habari ya baraza la serikali la China, Bw. Wei Hong amesema nyumba za wakulima ambazo zinajengwa au zimeshajengwa zinachukua asilimia 65 ya nyumba zinazohitajika kukarabatiwa; zaidi ya asilimia 40 ya shule zinazohitaji kukarabatiwa zinajengwa au zimeshajengwa; asilimia 96 ya makampuni yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi yameanza tena uzalishaji. Aidha, ukarabati wa hospitali, barabara na vifaa vya maji, mpango wa kufufua mazingira ya ikolojia, na ukarabati wa sehemu ambayo wanaishi panda unaendelea kutekelezwa.

Hali ya hewa ya sehemu za mkoa wa Sichuan zilizokumbwa na tetemeko la ardhi katika majira ya baridi ya mwaka huu ni baridi kali na yenye mvua nyingi. Bw. Wei alisema serikali itawasaidia wakazi wa huko kwa kuwapatia nguo, vyakula, nyumba na huduma za afya.