Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-21 18:21:25    
Undani wa "kumbukumbu" ya Kundi la Dalai Lama ni kutafuta njia ya kuifanya Tibet ijitenge kabisa na taifa la China

cri
Shirika la habari la China Xinhua tarehe 21 limetoa makala ya mchambuzi ikidhihrisha kuwa, "Kumbukumbu kwa ajili ya watibet wote wapate haki ya kujitawala kihalisi" liliyotawanya Kundi la Dalai Lama tarehe 16 Novemba nchini India, undani wake ni kutafuta njia ya kuifanya Tibet ijitenge kabisa na taifa la China. Makala hiyo imesema, kumbukumbu hiyo ilitetea "eneo kubwa wanakoishi watibet", "kujitawala kwenye kiwango cha juu" kwa mujibu wa katiba na sheria ya China, undani wake ni kujaribu kuanzisha kundi la siasa linalodhibitiwa na Kundi la Dailai Lama kwenye ardhi ya Tibet inayochukua robo ya ile ya jumla ya China, kundi hilo litakuwa la "nusu ya kujitawala" au la "kujitawala kwa njia tofauti", ili kutimiza lengo lake la kuifanya Tibet ijitenge kabisa na taifa la China. Makala hiyo imesema, serikali kuu ya China inafuata sera za siku zote juu ya Dalai Lama, na imefungua mlango wake zamani na siku za mbele kwa Dalai Lama ili arudi kwenye msimamo wa uzalendo, lakini serikali kuu haikufungua mlango zamani na pia haitafungua mlango siku za usoni kwa "kujitawala", au "nusu ya kujitawala" au "kujitawala kwa njia tofauti" kwa Tibet.