Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko ziarani nchini Peru tarehe 20 alitoa hotuba muhimu kwenye bunge la Peru, ambapo alisifu sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Latin Amerika, akisema China inapenda kufanya juhudi pamoja na nchi za Latin Amerika katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.
Katika hotuba yake rais Hu alidhihirisha kuwa, China inafuatilia maendeleo ya sehemu za Latin Amerika na Cariebbean. Mwaka 2004 alipofanya ziara katika nchi za Latin Amerika alisema, China ina matumaini kuwa China na nchi za Latin Amerika zitakuwa marafiki wa kutegemeka na wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo ya pamoja. Katika miaka minne iliyopita, maslahi ya pande hizo mbili yamehusiana karibu kiasi kwamba hali hiyo haikutokea hapo kabla, na hali kadhalika kiwango cha uhusiano kati ya pande hizo mbili. China na nchi za Latin Amerika zimekuwa marafiki wazuri na wenzi wema. Alisema:
China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na Latin Amerika ikiwa sehemu muhimu duniani inayoendelea, pande hizo mbili zinatakiwa kuungana barabara zaidi, na kuanzisha ushirikiano kwenye ngazi ya juu zaidi, sekta nyingi zaidi na kiwango cha juu zaidi, ushirikiano huo unalingana na mkondo wa zama tulizo nazo, pia unalingana na mahitaji ya maendeleo ya kila upande. Hapa nikiwa kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake nawaambia wote kwamba, China inapenda kujiunga pamoja na nchi za Latin Amerika na Cariebbean katika kujenga ushirikiano wa kiwenzi kwa pande zote ulio na usawa na kunufaishana na kutafuta maendeleo ya pamoja.
Rais Hu alisema, kujenga ushirikiano wa kiwenzi kati ya China na Latin Amerika kwenye sekta zote, ni lazima kutilia mkazo zaidi suala kuu la maendeleo ya pamoja. China inapenda kupanua ushirikiano halisi kati yake na nchi za Latina Amerika kwenye sekta mbalimbali, ili kusukuma mbele maendeleo ya kila upande katika ushirikiano huo; kufanya hivyo ni lazima kushikilia kanuni za kimsingi za kuwa na usawa na kunufaishana; China inapenda kupanua siku hadi siku maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili, kutafuta njia mpya ya ushirikiano, kupanua sekta za ushirikiano na kuongeza mambo ya ushirikiano.
Rais Hu alisema, China inapenda kufanya juhudi za pamoja na nchi za Latin Amerika katika mambo matano kama yafuatayo: kuendeleza zaidi uhusiano wa kisiasa, kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na ya ngazi mbalimbali, na kuongeza uaminifu wa kisiasa siku hadi siku; kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara; kuimarisha mawasiliano na kusawazisha misimamo kuhusu masuala makubwa ya dunia ili kulinda maslahi ya pamoja; kushiriki kwa pamoja kutunga kanuni za Kimataifa kuhusu uchumi, fedha na biashara ili kuhimiza utaratibu wa uchumi wa Kimataifa uendelee kwa mwelekeo wa haki na halali zaidi; kufundishana na kuigana katika kuhimiza maendeleo ya mambo ya jamii na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi; na kuongeza mazungumzo na maingiiano katika sekta ya utamaduni.
Alipozungumzia ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Latin Amerika, rais Hu alisema:
Tunatakiwa kutilia nguvu kuboresha miundo ya biashara, kuhimiza upanuaji wa biashara na maendeleo ya uwiano ya uhusiano wa kibiashara; kujitahidi kuongeza uwekezaji wa kila upande, kutilia mkazo uwekezaji na ushirikiano katika shughuli za utengenezaji, ujenzi wa miundo mbinu, nishati na madini, kilimo, na shughuli za sayansi na teknolojia za hali ya juu, pande mbili zinatakiwa kutoa sera na uelekezaji zaidi kuhamasisha makampuni ya pande mbili yaimarishe ushirikiano wa kimkakati katika biashara na uwekezaji na kutoa msaada zaidi; kushikilia mazungumzo yenye usawa ili kujadiliana kirafiki wakati wa kushughulikia kwa mwafaka matatizo halisi katika ushirikiano. Na China inapenda kuendelea kutoa misaada kadiri iwezavyo kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi za Latin Amerika na Cariebbean.
Mwishoni rais Hu Jintao alisifu sana mustakabali wa ushirikiano kati ya China na Latin Amerika.
|