Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-22 18:37:57    
Bw. Hui Liangyu asisitiza kuwa China inapaswa kuendelea kuimarisha sera za kuwanufaisha wakulima

cri

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Hui Liangyu hivi karibuni huko Jinan mkoani Shandong amesisitiza kuwa, China inapaswa kuendelea kuimarisha sera ya kuwanufaisha wakulima na kuweka mkazo katika kupanua mahitaji ya matumizi vijijini.

Bw. Hui Liangyu alisema, katika nusu ya pili ya mwaka huu, msukosuko wa fedha duniani umezidi kuathiri uchumi wa kilimo nchini China, bei ya mazao ya kilimo pia inaelekea kushuka, na kasi ya ongezeko la pato la wakulima imeanza kupungua.

Bw. Hui Liangyu alisema, China inapaswa kutilia maanani katika kupanua mahitaji ya matumizi vijijini, kuharakisha ujenzi wa miundombinu vijijini, kuharakisha ujenzi wa mazingira ya asili na ukarabati baada ya maafa, China pia inapaswa kujitahidi kuongeza pato la wakulima na kuboresha zaidi mazingira ya kazi na maisha ya watu vijijini.