Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-23 19:21:17    
China yaimarisha ujenzi wa mfumo wa huduma za matibabu na afya vijijini na ngazi ya shina

cri

Wizara ya afya ya China hivi karibuni ilitenga yuan bilioni 4.8 katika kuimarisha ujenzi wa mfumo wa huduma za matibabu na afya vijijini na ngazi ya shina.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Mao Anqun alisema, fedha hizo zitatumiwa kujenga hospitali na vituo vya afya zaidi ya 7,300 vijijini, na vituo vya afya karibu 6,000 kwenye sehemu za mashamba ya kilimo na misitu kwenye sehemu maskini za mashariki mwa China.

Imefahamika kuwa tangu mwaka 2004 China imejenga vituo vya afya zaidi ya elfu 32 vijijini.