Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 15:31:34    
Lima-Rais Hu Jintao wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kipindi cha pili wa viongozi wa APEC

cri

Mkutano usio rasmi wa kipindi cha pili wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC ulifanyika tarehe 23 huko Lima, Peru. Rais Hu Jintao wa China alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba kuhusu utandawazi wa uchumi wa kikanda, usalama wa binadamu na mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais Hu alipozungumzia utandawazi wa kikanda alisema kazi ya dharura ni kutimiza lengo la Bogor na kusukuma mbele mazungumzo ya duru la Doha la Shirika la Biashara Duniani.

Kuhusu usalama wa binadamu Rais hu alisema Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki inatakiwa kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kupunguza athari ya maafa, kufanya mazungumzo kuhusu sera, kubadilishana maarifa na kuimarisha msaada wa teknolojia.

Rais Hu alipozungumzia mabadiliko ya hali ya hewa alisema China ina matumaini kuwa pande mbalimbali zitafanya juhudi kwa pamoja za kutunga mpango wenye ufanisi, ili kuimarisha utekelezaji wa makubaliano ya mpango wa Bali.