Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 19:12:41    
Zurich-Shirika la fedha duniani lasema msukosuko wa fedha duniani utaendelea kuwa mbaya

cri
Mtaalam mkuu wa Uchumi wa Shirika la Fedha duniani IMF Bw. Olivier Blanchard tarehe 22 huko Zurich, mji wa Switzerland alisema, shirika hilo halina uwezo wa kutatua mzunguko wa fedha usio wa kutosha kwenye mfumo wa fedha, na msukosuko wa fedha duniani utaendelea kuwa mbaya.

Bw. Blanchard alipohojiwa na vyombo vya habari vya Switzerland alisema, tangu msukosuko wa fedha utokee hadi hivi sasa, Shirika la fedha duniani limetoa misaada ya mikopo kwa nchi za Iceland, Latvia, Hungari na Pakistan. Wiki mbili zilizopita, shirika hilo limetumia 25% ya jumla ya dola bilioni 250 za Marekani. Alibashiri kuwa msukosuko wa fedha utaendelea kuwa mbaya, hivyo kukabiliana na msukosuko huo kunahitaji muda, na alikadiria kuwa ni vigumu kufufuka kwa hali ya fedha duniani mpaka mwaka 2010.