Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 19:38:33    
Uwekezaji mpya wa yuan bilioni 100 hautasababisha ujenzi wa marudio na uwekezaji ovyo

cri

Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Mu Hong tarehe 24 hapa Beijing amesema, serikali kuu ya China itazuia ujenzi wa marudio na uwekezaji ovyo kutokana na nyongeza za uwekezaji wa yuan bilioni 100, kwa kupitia kuongeza usimamizi na kufanya ukaguzi wa pamoja.

Bw. Mu Hong amesema ili kuhakikisha miradi ya nyongeza za uwekezaji inaanzishwa, na kutekelezwa haraka iwezekanavyo, kikundi cha uongozi wa kazi ya kukagua utekelezaji wa sera ya serikali kuu ya kupanua matumizi ya ndani na ongezeko la uchumi kitawatuma wajumbe wake kwenye mikoa 31 nchini China.

Imefahamika kuwa uwekezaji huo hasa utatumiwa katika miradi ya ujenzi wa miundo mbinu, kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa uchafu na ujenzi wa kuhifadhi mazingira ya asili.