Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 19:40:18    
Kinshasa-Rais wa zamani wa Zambia asema China inaweza kufanya kazi muhimu katika ukarabati wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

cri

Gazeti la Posta la Zambia tarehe 23 ilitoa makala ya rais mstaafu wa Zambia Bw. Kenneth Kaunda, ikiona kuwa China inaweza kuonesha umuhimu wake katika ukarabati wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwenye makala hiyo iitwayo Tafadhali kuiacha China Isaidie Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bw. Kaunda aliisifu sana serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuongeza ushirikiano na China katika miaka ya hivi karibuni, na kuyaalika makampuni ya China kushiriki kwenye kazi za ukarabati nchini humo.

Bw. Kaunda alisema miradi inayotekelezwa na makampuni ya China si kama tu inaboresha hali ya miundo mbinu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, bali pia inaongeza nafasi ya ajira kwa watu wa nchi hiyo.