Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 19:55:56    
Athens-Rais wa China aanza ziara rasmi nchini Ugiriki

cri

Kutokana na mwaliko wa rais Karolos Papoulias wa Ugiriki, rais Hu Jintao wa China alasiri ya tarehe 24 amefika huko Athens, na kuanza ziara yake rasmi nchini Ugiriki.

Kwenye hotuba yake ya maandishi aliyoitoa kwenye uwanja wa ndege, rais Hu amesema mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Ugiriki na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo zina historia ndefu, katika miaka ya hivi karibuni msingi wa uhusiano wa kimkakati na kiwenzi katika sekta mbalimbali kati ya China na Ugiriki unaimarishwa siku hadi siku, mawasiliano na ushirikiano kati yao katika nyanja mbalimbali zinaendelea kwa kasi, China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano kati yake na Ugiriki, na inapenda kushirikiana na nchi hiyo kuanzisha mustakabali mzuri zaidi wa uhusiano huo. Rais Hu ameeleza imani yake kuwa, chini ya juhudi za pande hizo mbili, ziara yake hiyo itahimiza uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Ugiriki uendelezwe zaidi.