Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-24 21:33:55    
Jerusalem- Bw. Mahmoud Abbas achaguliwa kuwa rais wa Palestina

cri

Kamati kuu ya chama cha ukombozi cha Palestina PLO tarehe 23 ilifanya mkutano mjini Ramallah, magharibi mwa Mto Jordon, ambapo ulimpitisha kwa kauli moja Bw. Mahmoud Abbas kuwa rais wa Palestina.

Bw. Abbas hivi sasa anashika nyadhifa za mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya chama cha ukombozi cha Palestina, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Paletina, pia ni kiongozi wa Kundi la Fatah ambalo ni moja kati ya makundi makubwa ya kisiasa ya Palestina. Kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Palestina kunamaanisha kuwa, Bw. Abbas ameshika nyadhifa zote muhimu alizoshika kiongozi wa zamani wa Palestina marehemu Yasser-Arafat.

Kamati kuu ya PLO ina wajumbe zaidi ya 100 ambao walichaguliwa na Halmashauri  ya taifa ya Palestina, ni mamlaka ya usimamizi kati ya Halmashauri  ya taifa ya Palestina na kamati ya utendaji ya PLO.