Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 14:41:55    
Bukavu- Bw. Ban Ki-moon aomboleza kifo cha mwandishi wa habari wa Radio aliyeuawa

cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 24 alitoa taarifa akieleza kuomboleza kifo cha mwandishi wa habari wa Radio Okapi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyepigwa risasi huko Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kusini Kivu.

Bw. Ban Ki-moon alisema tukio hilo limeonesha tena kuwa hali ya usalama wa nchi hiyo sio tulivu sana, kutokana na umaalumu wa kazi ya uandishi wa habari, usalama wao ni vigumu kuhakikishwa.

Bw. Ban Ki-moon aliitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ifanye uchunguzi kikamilifu juu ya tukio hilo, na kusema tume maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini humo inafuatilia maendeleo yatakayopatikana katika uchunguzi huo, na inapenda kutoa misaada yote ya lazima ili kukamilisha haraka uchunguzi na hukumu.