Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 14:45:47    
Viongozi wa serikali na chama wa Afrika Kusini wakutana na Liu Qi

cri
Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC cha Afrika kusini Bw. Jacob Zuma na rais Kgalema Motlanthe wa Afrika Kusini tarehe 24 huko Johannesburg walikutana na ujumbe ulioongozwa na Bw. Liu Qi ambaye ni mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na katibu wa kamati ya Chama ya Beijing.

Bw. Liu Qi alitoa salamu za katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na rais wa China Bw. Hu Jintao kwa Bw. Jacob Zuma na Bw. Kgalema Motlanthe, Bw. Liu Qi alisisitiza kwamba Chama cha Kikomunisti cha China kinathamini sana uhusiano wa kirafiki kati yake na chama cha ANC na kupenda kufanya juhudi pamoja na ANC ili kuimarisha maingiliano na ushirikiano wa aina mpya kati ya vyama viwili na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa pande zote.

Ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China tarehe 22 ulifika Afrika Kusini kufanya ziara rasmi kutokana na mwaliko wa chama cha ANC.